Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Wednesday, November 2, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA NAIROBI SOUTHERN BYPASS KATIKA ENEO LA KAREN NCHINI KENYA, ATEMBELEA KIWANDA CHA MAZIWA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wakiserebuka na wanakwaya katika eneo la Karen mara baada ya kufungua barabara “mchepuko” ya (Nairobi Southern Bypass), nchini Kenya Novemba 1, 2016.  (PICHA NA IKULU)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Naibu Rais wa Kenya William Rutto pamoja na viongozi wengine, wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya kupunguza msongamano ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Bi. Lucy Karuga kuhusu usindikaji wa mazao ya chakula katika kiwanda cha Maziwa cha Eldoville katika eneo la Karen nchini Kenya.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia usindikaji wa Samli katika kiwanda hicho cha maziwa cha Eldoville nchini Kenya.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Ngina Kenyatta mama mzazi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati alipomtembelea nyumbani kwake Nairobi nchini Kenya.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mama Ngina Kenyatta mama mzazi wa Rais Uhuru Kenyatta pamoja na Rais Uhuru Kenyatta wakati alipomtembelea mama huyo nyumbani kwake Nairobi nchini Kenya.

0 comments: