Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Thursday, March 29, 2012

MH BALOZI DKT BATILDA S. BURIANI AWASILISHA HATI ZAKE ZA UTAMBULISHO KWA MH. RAIS MWAI KIBAKI



 Mh. Balozi Dkt Batilda S. Burian, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya, amewasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mh. Mwai Kibaki, Rais wa Jamhuri ya Kenya tarehe 28 Machi, 2012. Hafla hiyo fupi iliandaliwa IKULU, Nairobi. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mh. Prof. Sam Ongeri, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na viongozi wengine wa Serikali. Pichani juu Mh. Balozi Dkt Batilda S. Burian akisoma hotuba fupi ya kuwasilisha rasmi Hati zake za Utambulisho kwa Mh. Rais Mwai Kibaki.
 Mh. Balozi Dkt Batilda S. Burian akikabidhi rasmi Hati zake za Utambulisho kwa Mh. Rais Mwai Kibaki.
 Mh. Balozi Dkt Batilda S. Burian akitambulisha rasmi ujumbe wake aliombatana nao. 
 Mh. Rais Mwai Kibaki akiteta jambo na Maafisa wa Ubalozi alioambatana nae.  Kutoka kushoto kwa Mh. Rais ni Bw. Innocent Eugene Shiyo, Mkuu wa Utawala na Fedha ambaye pia anasimamia Masuala ya Uchumi na EAC, Brig Gen Edwin Victor Millinga, Mwambata Jeshi, Bi Grace Mgovano, Mkuu wa Kitengo cha Siasa na Bibi Kemilembe Mutasa, Mwambata Mazingira.

Mh. Rais Mwai Kibaki akiteta jambo na Mh. Balozi Dkt Burian kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na Mh. Rais kwa ajili  ya Mabalozi waliowasilisha Hati zao.
Picha na Michuzi Blog

0 comments: