Social Icons

Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Featured Posts

Wednesday, July 26, 2017

MAMA SALMA KIKWETE ASHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA KAMUSI KUU YA KISWAHILI NCHINI KENYA

 Balozi wa Kiswahili Afrika Mama Salma Kikwete akiongea wakati wa uzinduzi wa Kamusi Rasmi ya Kiswahili nchini Kenya katika Jengo la Kenya Institute of Curriculum Development, Nairobi, Kenya ambapo ameahidi kuitumia kwa manufaa ya Tanzania, Kenya, Jumuiya ya Afrika Mashariki,  Afrika na Duniani kwa Ujumla.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea wakati wa uzinduzi wa Kamusi Rasmi ya Kiswahili nchini Kenya katika Jengo la Kenya Institute of Curriculum Development, Nairobi, Kenya.
Balozi wa Kiswahili Afrika Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania, Kenya, Dkt. Pindi Chana (wa kwanza kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) wakati wa uzinduzi wa Kamusi Rasmi ya Kiswahili leo nchini Kenya.

FRANCIS DAMIANO DAMAS ASHINDA MEDALI YA SHABA MASHINDANO YA VIJANA YA JUMUIYA YA MADOLA NCHINI BAHAMASKijana Francis Damiano Damas (17)  ametwaa medaili ya shaba katika mbio za mita 3000  kwenye  mashindano ya sita  vijana kutoka  nchi za Jumuiya ya Madola yaliyomalizika mwishoni mwa juma jijini  Nassau nchini Bahamas. Picha ya juu inamuonesha Kijana Francis Damiano Damas akiwa na wenzake Collins (kushoto) Kiongozi wa msafara Mwinga Mwanjala (katikati), kulia ni Celina Itatiro (14) na wa pili kulia ni Regina (15)


SPIKA NDUGAI AHUDHURIA MKUTANO WA MASPIKA WA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA BARANI AFRIKA JIJINI ABUJA, NIGERIA


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akitambulishwa katika mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika unaofanyika Abuja Nigeria.Mkutano huo unafanyika kujadili masuala mbali mbali yanayohusu mabunge hayo unashirikisha Maspika toka nchi 18 za Jumuiya ya Madola Barani Afrika.

Monday, July 24, 2017

MSIBA MAREKANI
Tarifa za kusikitisha za kifo cha mwenzetu Peter M Jennings Kessy. Mtanzania alikuwa akiishi Bronx New York kilichotokea siku   July11,2017 .
Ndugu Peter Jennings ni mjomba wa Rose Gadner wa Connecticut . Taratibu za mazishi zinapangwa ambapo mwili utasafirishwa kuelekea nyumbani Kilimanjaro -Tanzania.Kabla ya kusafirishwa mwili utaangwa August 12,2017(Tentative ) .
Kama ilivyo ada yetu tushirikiane ktk kipindi hiki kigumu ,tuonyeshe umoja, upendo na udugu wetu kwa hali na mali. Tunawaombea Mungu awape nguvu na faraja.
Pole kwa ndugu , jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.

Taarifa zaidi zitatolewa kadiri zitapokuwa tayari au wasiliana na :
Rose Gadner:+12038140545More contacts &
info to follow #UpdatesAsWeGet

Aksanteni,


Sylvester Mwingira.
Hi everyone, please click here to support my GoFundMe campaign, Peter's Tanzania Funeral Fund: 

Chanzo Michuzi Blogu


Tuesday, July 4, 2017

BALOZI MODEST MERO AMPONGEZA KANALI GEORGE ITANG'IRE KWA KUPANDISHWA CHEOBalozi na Mwakilishi Mkazi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Modest Mero akimpongeza Kanali George Itang'ire kwa kupandishwa cheo na Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli kutoka ngazi ya Luteni Kanali na kuwa Kanali wa JWTZ katika ofisi za ubalozi wa Tanzania jijini New York leo.
Picha kwa hisani ya Michuzi blog


Monday, July 3, 2017

MAKAMU WA RAIS MH SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI JIJINI ADDIS ABABA USIKU HUU KUMUWAKILISHA RAIS KATIKA MKUTANO WA 29 WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI YA UMOJA WA AFRIKA (AU).


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili usiku huu Jijini Addis Ababa, Ethiopia ambapo hapo kesho tarehe 03 Julai 2017 atahudhuria Mkutano wa 29 wa Wakuu wa  Nchi na Serikali  wa Umoja wa Afrika (AU).Mhe.Samia amepokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Ethiopia Pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Naimi Aziz na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Augustine Mahiga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Augustine Mahiga mara baada ya kuwasili jijini Addis Ababa,nchini Ethiopia usiku huu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassa akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili jijini Addis Ababa mapema usiku huu


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili usiku huu Jijini Addis Ababa, Ethiopia ambapo hapo kesho tarehe 03 Julai 2017 atahudhuria Mkutano wa 29 wa Wakuu wa  Nchi na Serikali  wa Umoja wa Afrika (AU).

Katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Ethiopia Pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Naimi Aziz na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Augustine Mahiga.

Katika Mkutano huo wa siku mbili kuanzia tarehe 03-hadi 04 Julai-2017, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan atamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo.

 Kabla ya ufunguzi rasmi, Mkutano huo ulitanguliwa na vikao vya Baraza la Utendaji linalowashirikisha Mawaziri wa Mambo ya Nje na Kamati ya Uwakilishi wa Kudumu  inayowahusisha Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje kutoka nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika.

Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi  na Serikali  utafunguliwa rasmi kesho tarehe 03-Julai-2017 katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika Jijini Addis Ababa, Ethiopia na  utajikita katika kujadili masuala mbalimbali yanayohusu umoja huo.

Miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika Mkutano huo ni pamoja na taarifa  kuhusu Maboresho katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na maboresho ya kitaasisi katika AU na  hali ya Ulinzi na Usalama katika bara la Afrika.

Kuhusu  hali ya  ulinzi na usalama katika Bara la Afrika majadiliano ya Viongozi hao yatajikita zaidi kwenye nchi za Sudan Kusini, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- DRC na Libya.  Aidha, majadiliano hayo pia yatagusa  hali ya usalama kwenye baadhi ya nchi ambazo ziliathiriwa na kundi la Boko Haram za  Nigeria, Niger, Chad na Cameroon.

Mkutano huo 29 wa AU, unatarajiwa kuhuduhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.

Mkutano huo 29 wa AU utakaofanyika Jijini Addis Ababa, Ethiopia utaongozwa na Mheshimiwa  Alpha Conde  Rais wa Jamhuri ya Guinea ambaye ndiye Mwenyekiti wa AU.

Kauli Mbiu ya Mkutano huo ni Kuimarisha Mgawanyiko wa Idadi ya Watu Kupitia Uwekezaji katika Vijana (Harnessing Demographic Divident Through Investments in the Youth)

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 ADDIS ABABA- ETHIOPIA.      

03-Julai-2017
 

Thursday, June 29, 2017

TAMCO KUENDELEZA HARAKATI ZA KIDINI, KIJAMII TANZANIA

Na Swahilivilla, Washington
Jumuiya ya Waislamu wa Tanzania waishio katika jiji la Washington na vitongoji vyake (TAMCO), imejidhatiti kuendeleza harakati za kijamii nchini Tanzania.
Mweka Hazina  wa Jumuiya ya Waislamu wa Tanzania  (TAMCO), Bi Asha Hariz 
Hayo yalielezwa na Mweka Hazina wa Jumuiya hiyo Bi Asha Hariz katika mazungumzo maalum na Swahilivilla pembezoni mwa Sherehe za Idd Al-Fitri zilizoandaliwa na jumuiya hiyo kuadhimisha kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika Mji huo Mkuu wa Marekani.
Katika Sherehe hizo zilizohudhuriwa na Balozi Mstaafu Bwana Mustafa Nyang'anyi, Bi Asha alisema kuwa, kwa kupitia Kamati yake ya Uhamasishaji, TAMCO imekuwa ikifanya juhudi za kusaidia katika shughuli kama za ujenzi wa Misikiti na vituo vya mayatima nchini Tanzania.
Alitoa mfano wa ujenzi wa Msikiti katika Mkoa wa Simiyu uliofadhiliwa na jumuiya hiyo akisema: " Kule Simiyu, Waislamu wenzetu walikuwa wana ardhi tu, lakini walikuwa hawajui jinsi ya kuiendeleza. Alhamudu Lillah, Mwenyezi Mungu ametuunganisha nao, na wanachama wetu wakajitolea kwa michango, na kuwasaidia kusimamisha Msikiti"
Wanafunzi waanza masomo ya Darsa, ndani ya  Msikiti wa Simiyu
TAMCO haikusitisha juhudi zake baada ya kusimama kwa kuta za Msikiti huo tu, bali iliendeleza juhudi ili kuhakikisha kuwa Msikiti huo unakuwa na huduma zote muhimu ikiwemo nishati ya umeme.
"Baada ya Msikiti kusimama, bado kulikuwa na haja ya Msikiti huo kuwa na huduma ya umeme, nasi tukafanya juhudi za michango tukawatumia, na sasa Msikiti huo una umeme", alisema Mweka Hazina wa TAMCO.
Mbali na huduma kama hizo za majengo ya ibada, Bi Asha Hariz aliendelea kufafanua kuwa Jumuiya yake inaendesha vituo vya Mayatima nchini Tanzania.
"Sasa hivi tuna mradi mwengine wa kuwasaidia watoto mayatima. Tuna kituo pale Tandale, Dar es Salaam, na chengine Kibaha, kwa hivyo wale watoto nao pia tunawasidia." Alifafanua.
Image may contain: one or more people
TAMCO Zakatul Fitri kwaajili ya kusaidia Tanzania Aliongeza kusema: "Na katika kipato chengine tunachokusanya ni Zakatul Fitri, ambazo kwa mwaka huu tumepeleka Zanzibar - Unguja na Pemba ili kuwasaidia wanawake wenye uwezo mdogo wa kiuchumi. Na sehemu nyengine ya Zaka hiyo tumeipeleka kwenye vituo vyetu vya mayatima na Simiyu".

Mahojiano ya Mubelwa Bandio na Shose Kombe kuhusu Diaspora

Karibu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio na Mkuu wa Mawasiliano wa Diaspora kutoka KCB Bank Shose Kombe.
Mahojiano haya yalifanyika ndani ya Kilimanjaro Studio iliyopo Beltsville, Maryland nchini Marekani

Wednesday, June 28, 2017

SHEREHE ZA EID EL FITR DMV ILIYOANDALIWA NA TAMCO YAFANA


Mwenyekiti wa TAMCO (Jumuiya ya Waislamu DMV) Bwn Ally Mohamed akitoa salamuza Eid El Fitr kwa Waislam na marafiki zao DMV kwenye sherehe ya Eid El Fitr iliyofanyika siku ya Jumapili June 25, 2017 Silver Spring, Maryland.Picha na Vijimambo Blog na Kwanza production.
Kushoto ni Balozi Mustafa Nyang"anyi akijumuika kwenye sherehe ya Eid El Fitr na Watanzania DMV.
Balozi Mustafa Nyang"anyi akifuatilia sherehe ya Eid El Fitr iliyofanyika Sliver Spring, Maryland siku ya Jumapili June 25, 2017, kulia ni Seif Ameir.
Watanzania DMV wakijumuika pamoja katika sherehe ya Eid El Fitr iliyofanyika Silver Spring, Maryland siku ya Jumapili June 25, 2017.


 


-- visit my blog at http://lukemusicfactory.blogspot.com/