Ile sherehe ya Muungano wa Tanzania na Utamaduni wa Tanzania ambayo kila mwaka inaandaliwa na Jumuiya ya Watanzania Roma mjini Rome, na kusherekewa na Watanzania wote nchini Italy mwaka huu itafanyika siku ya Jumamos tarehe 28 april 2012 kuanzia saa kumi na moja jioni mpaka Lyamba, kwenye ukumbi wa KARISPERA CLUB 69 ulipo kwenye mtaa wa VIA ANGELO EMO 69, mjini Roma.Kutokana na ombi la Watanzania wengi, Mwaka huu sherehe hizi zitasherekewa mpaka usiku mnene.Uongozi wa Jumuiya unapenda kuwajulisha Watanzania wote waishio Rome na Italy kwa ujumla kuwa mnaomba muwasiliane na Mwenyekiti wa jumuiya Mh.Leonce au katibu ndugu Andrew Chole Mhella kupitia e-mail hii www.watanzaniaroma.yahoo.it au kwa simu namba 0039-3479094800 ili muweze kupata taratibu za kushiriki kwenye sherehe hii.Uongozi unawaomba pia Watanzania wote mfike kwa wingi kwenye kikao cha mwisho ili kuweza kuweka mambo sawa kabla ya sherehe. Mkutano utafanyika jumamosi ijayo tarehe 21 aprili kwenye Mtaa wa Via Principe Amedeo 70, uliopo maeneo ya Termini Station.Kwa maelezo zaidi tutembeleeni hapa
Andrew Chole Mhella,
Katibu.
0 comments:
Post a Comment