Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Sunday, November 25, 2012

WATANZANIA NEW YORK WALIVYOMUAGA MTOTO JESCA EMMANUEL



Watanzania wanaoishi jijini New York na Vitongoji vyake wakiwamo wawakilishi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, jana Jumamosi, waliungana na Familia ya Bw. Emmanuel Alfred Swere na Bi. Doto na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, katika Ibada ya kumuaga Jesca Emmanuel (12) aliyefariki ghafla Jumapili iliyopita.

 Ibada ya kumuaga Jesca ilifanyika Bergen Funeral Home na iliongozwa na Mchungaji Perucy Butiku. Mazishi ya Marehemu Jesca yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne katika kijiji cha Bumbombi- Tarime Tanzania. Raha ya Milele Umpe Eee Bwana na Mwanga wa Milele Umuangazie Apumzike kwa Amani. Amina
Mama mzazi wa Jesca  Bi. Doto akilia kwa uchungu mara baada ya kuona  mwili wa mtoto wake.
Baba  mzazi wa  Jesca, Bw. Emmanuel akilia kwa  uchungu mara baada ya kumwona mtoto wake, pembeni yake ni Shangazi wa Jesca, Bi. Rose
 Mchungaji Perucy Butiku akiongoza Ibada ya  kumuombea Marehemu Jesca Emmnauel na kuwafariji wazazi wake, ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwakumbusha waombolezaji kwamba kila mmoja wetu anasiku yake atakayoitwa na  Mwenye-Enzi Mungu,  kama alivyoitwa Mtoto  Jesca, ni siku ambayo hakuna mtu aijuaye. Na kwa sababu hiyo akasisitiza  umuhimu wa kujianda. Ibada ilifanyika siku ya Jumamosi Bergen Funeral Home jijini New York.
 Mdogo wake Jesca, Catherine akiwa ameelemewa na majonzi mazito kwa kuondokewa na dadayake, Catherine  aliwatia uchungu waombelezaji pale alipomuaga  Dada yake kwa  kutamka  "  Bye Jesca". 
Brigedia Jenerali Maganga Mwambata Jeshi  katika  Ubalozi wa Tanzania nchi Marekani, akiaga. Brigedia Jenerali Maganga ni kati ya   Maafisa  wanne waliowakilisha  wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
 Balozi   Tuvako  Manongi   akiungana na waombelezaji wengine  kumuaga marehemu Jesca. Baada ya  ratiba ya kuaga,  Balozi Manongi aliwashukuru watanzania kwa ushirikiano, upendo na mshikamano mkubwa waliouonyesha wakati wote wa kipindi cha maombolezo ya msiba huo na akawasihi kuendeleza umoja huo

 Bw. Emmanuel na Bi.  Doto wakiwa na mtoto wao,  muda mfupi kabla ya sanduku kufungwa 
Sanduku   lenye mwili wa Jesca tayari kwa Safari ya kwenda  Bumbombi- Tarime Tanzania kwa Mazishi.  

0 comments: