Freddy Mtoi

Coffin bearers walk out- Charles Hillary watches

Coffin- females sing past.

Blogger Prochest Tairo

Salim Kikeke with Simon Mziwanda

Freddy Macha(right) with Zawadi Machibya-co-ordinator of memorial service.
--
“Alikua mfano dhahiri wa neno
mtanashati”
mtanashati”
-Zawadi Machibya, mratibu wa
msiba na mtangazaji wa BBC Swahili
msiba na mtangazaji wa BBC Swahili
Na Freddy Macha
Kanisa la St Annes Lutheran katikati ya jiji la London
juzi Jumamosi lilikuwa kituo maalum cha kumwaga na kuwa wasifu wa maisha
ya marehemu Freddy Alex Mtoi aliyekuwa mtangazaji wa BBC Swahili kwa
miaka mingi.

Ibada hiyo iliyoendeshwa na wachungaji Tumaini
Kalaghe na Mathew Jutta, ilihudhuriwa na wanahabari mbalimbali kutoka
BBC , Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania, Clement Kiondo, marafiki wa karibu
waliomjua marehemu na wanananchi wa sehemu toka Tanzania, Afrika na
Ulaya.

Mratibu wa mazishi , Zawadi Machibya, ambaye ni mtangazaji
wa BBC, aliendesha shughuli na kuwajulisha wasemaji wote waliozungumzia
kwa kuanza kueleza namna neno “mtanashati” lilivyomvaa Freddy Mtoi
aliyefariki usiku wa kuamkia Jumamosi tarehe 17 Novemba, 2012.

Mchungaji Mathew Jutta alikumbusha kwamba safari
yetu wanadamu huanzia kwa Mungu na kuishia kwa Mungu. Akailinganisha
nsafari hiyo na ile ya kutoka nyumbani Afrika kuja Majuu (ambapo paliitwa
Mtoni enzi mchungaji alipokuja Ulaya takribani miaka 20 iliyopita).
“Kwa wanaobakia ni huzuni lakini kwa anayesafiri ni furaha yenye matumaini.”
Akimzungumzia marehemu alitaka zaidi kututuliza roho tuliyobakia.

Maneno haya yalisimama dede kama dhamira kuu ya msiba.
Kwamba badala ya kuhuzunika tujiratayarishe tunakokwenda kwa kuzingatia
maneno ya Biblia, Yohana Mtakatifu 3:20 : “ Maana kila mtu atendaye
mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.”

Wafanyakazi wenzake marehemu Mtoi nao waliendeleza
hoja kwa kutueleza undani wa bidii yake marehemu kazini, tabia yake
ya uungwana na upole. Akifafanua kwa kina, mtangazaji wa BBC toka
Kenya Solomon Mugera alitoa mfano namna marehemu alipokuwa tayari kumenyeka
hata wakati wenzake wakitaka kupumzika kama wakati wa sikukuu ya Krismasi.
Mugera :“ Marehemu hakuwa mlalamishi au mbishi. Alikua haogopi kufanya
kitu ambacho hakifahamu.”

Akitoa maelezo katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza
kwa niaba ya wageni wengine, Solomon alitaja mfano mwingine mkubwa wa
jinsi Mtoi alivyokua mchapa kazi asiyenung’unika kiasi ambacho hata
alipokuwa mgonjwa aliwaambia wenzake “ni kitu kidogo tu” wasitie
shaka, kumbe mwenzetu alikua akielekea katika kifo.

Salim Kikeke mtangazaji gwiji aliyefanya kazi
na marehemu toka Bongo miaka kumi iiliyopita alitukumbusha zaidi kwa
undani vipindi Freddy Mtoi alivyovitoa kwa kuacha sauti yake isikike
kwa wastani wa dakika moja. Hapo tulimsikia akiwahoji wananchi mbalimbali
mitaani Uingereza. Mfano kipindi alichowauliza watu maana ya mti wa
Krismasi, unaothaminiwa sana na Wazungu. Kati ya wahojiwa alikuwa mchungaji
Tumaini Kallaghe aliyeongoza sala hii juzi.

Tulipata vile vile fursa ya kusikiliza sauti za wazazi
wake Mtoi wakieleza namna alivyokuwa mtoto mwenye bidii, mtiifu na aliyeanza
kuipenda kazi ya uanahabari toka angali mdogo sana.

Mbali na wafanyakazi walikuwepo pia marafiki zake
wa karibu , mathalan Prochest Tairo aliyefuta dhana iliyoenea ( toka
msiba ulipotokea) kwamba marehemu alikuwa msiri na mtu wa kujificha.

Tairo ambaye pia ni bloga na alimjua Mtoi toka wakisoma
wote sheria chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1997- 2002 alisema:
“Kwa nje alikuwa akionekana mkimya sana, mkiongea anasikiliza anatabasamu.
Lakini ukishamzoea ni mzungumzaji sana...si kweli alikuwa mkimya, ila
ilibidi akuzoee.”

Aliongeza kueleza marehemu alipenda mazoezi ya viungo.
Siku moja walikuwa mahali hadi ikafika usiku sana, lakini marehemu alitaka
awahi Gym afanye angalau mazoezi nusu saa kabla ya kuelekea nyumbani.
Wengi hatukujua alikuwa mpenda mazoezi.

Ibada iliendelea kwa nyimbo, sala na wahudhuriaji
kutoa heshima zetu za mwisho mbele ya jeneza, kabla ya kusafirishwa
Dar es Salaam, leo Jumatatu.

Idhaa ya BBC Swahili ambayo ilihusika sana na matayarisho
haya ikisaidiana na Israel Saria, mwanahabari wa michezo anayeendesha
tovuti ya Tanzania Sports, iliwakilishwa na watangazaji wengi maarufu
wakiwemo pia Charles Hillary, Idi Sefu, Zuhura Yunus na Peter Musembi.

Akitoa neno lake Israel Saria alisema alijuana na
Freddy Mtoi toka Tanzania. Saria ataisindikiza maiti inayotarajiwa kuwasili Dar es Salaam
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kwa ndege ya British
Airways, Jumanne saa moja asubuhi.

Mipango ya Ibada na mazishi Tanzania itafanyika nyumbani kwa wazazi
wake Tabata Maduka Manne jijini Dar es Salaam, saa Saba mchana Jumatano.
Mazishi yatafanyika makaburi ya Kinondoni
, Jumatano hiyo hiyo saa tisa alasiri.
Habari zaidi tembelea:
www.kitoto.wordpress.com
0 comments:
Post a Comment