Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Wednesday, May 22, 2013

TAARIFA YA MSIBA DMV NA TANZANIA



Martin Ngireu Enzi ya Uhai Wake
Familia ya Ngireu inasikitika kutangaza kifo cha mpendwa baba yao Martin Ngireu kilichotokea siku ya Jumanne May 21, 2013 katika Hospitali ya Holy Cross iliyopo Silver Spring, Maryland, nchini Marekani.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Donalson Funeral Home, iliyopo 313 Talbot Avenue, Laurel MD na kutakua na Misa na kumuaga marehemu siku ya Jumamosi May 25, 2013 kuanzia saa 6 mchana mpaka saa 10 jioni (12-4pm) kwenye addres 313 Talbot Avenue, Laurel, MD baada ya hapo kutakua na chakula kwenye address 210 Patuxent Road, Laurel MD

Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu inafanywa na kama ilivyodesturi yetu kupena pole ndio ustaarabu wetu Msiba upo 210 Patuxent Road, Laurel MD kwapa pole watoto wa marehemu Carol na dada yake waliokuja kutoka Tanzania. Msiba huu ni wetu sote DMV tafadhali tujumuike na tuwafiriji wafiwa. Kushirikiana na kushikamana kwa shida na raha ndio staili na maisha yetu DMV.
Kwa maelezo na maelekezo tafadhali wasiliana na Mtoto wa Marehemu Carol 301 957 4523.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe.

0 comments: