Ubalozi wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania London unawakaribisha Watanzania wote watakaoweza kupata
fursa kuja kuzungumza na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda
hapo Ubalozini siku ya Jumanne (tarehe 6 Agosti 2013) kuanzia saa Kumi na Nusu
alasiri (1630 hours au 04.30 p.m.).
Katika Mkutano huo,
Mheshimiwa Pinda anatarajiwa kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo ya
nchi na ushirikishwaji wa Diaspora. Aidha atajibu maswali kutoka kwa wananchi
hao.
IMETOLEWA
NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA, LONDON, JUMAPILI (4 AGOSTI 2013)
0 comments:
Post a Comment