Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Monday, October 28, 2013

HISIA AZIDI KUPETA TUSKER PROJECT FAME: Angel ahitaji sapoti ya watanzania ili kuendelea kupeperusha bendera ya nchi yetu.

 Baadhi ya washiriki wa shindano la Tusker Project Fame msimu wa sita wakisikiliza kwa makini maelekezo ya watangazaji wa kipindi hicho(hawapo pichani)kutoka kushoto ni mshiriki kutoka Tanzania Hisia, Hope kutoka Burundi na Bior kutoka Sudan ya Kusini
 Mmoja wa washiriki kutoka Tanzania aliyeingizwa kikaangoni Angella Karashani(Angel)akimiliki jukwaa katika kipindi cha tatu cha Tusker Project Fame msimu wa sita huku akiimba kibao cha‘Don’t You Remember’ chake Adele Jumapili jijini Nairobi.
 Mmoja wa washiriki wanaoiwakilisha vyema Tanzania Elisha Maghiya(Hisia)akimiliki jukwaa katika kipindi cha tatu cha Tusker Project Fame msimu wa sita huku akiimba kibao cha `Here I Stand’ chake Usher Jumapili jijini Nairobi.

28 Oktoba 2013, Ni baada ya vuta nikuvute katika kinyaganyiro cha shindano la vipaji vya kuimba maarufu kama Tusker Project Fame kipindi cha tatu ambapo kila mshiriki alikuwa amejinoa vya kutosha ili kuhakikisha anaendelea kubaki katika mashindano hayo. Wawakilishi wa  nchi yetu Angel na Hisia walionekana kufanya vyema huku Hisia akipagawisha zaidi.

Mashindano yalianza huku kila mmoja akionesha kuwa na shauku kubwa hasa Bior, Fessy pamoja na Jennifer ambao walinusurika katika hatari ya kutolewa katika mashindano hayo baada ya kuwa wamerudia nyimbo zao siku ya jumamosi na kufanikiwa kubaki katika shindano hilo. Mishel kutoka Kenya pamoja na Under Coverbrothers kutoka Uganda waliaga mashindano hayo siku ya jumamosi.

Angel alimiliki jukwaa mara baada ya Patrick kufungua zoezi hilo. Akiwa amevalia gauni nyekundu iliyokuwa ikionesha wazi muonekano mzuri alionao huku ikimstiri vizuri aliimba wimbo wa ‘Don’t You Remember’ wa Adele.  Alifanya vizuri huku akishangiliwa na mashabiki  waliovutiwa na hisia zake katika kuimba wimbo huo. Majaji walionekana kutoridhirishwa sana na uimbaji wake wakimtaka aongeza jitihada kwani sauti ya kuimba anayo na anaweza, kikubwa ni kuongeza bidii.

Hisia nae alionyesha umahiri wake katika kuitumia sauti, kujiamini na kulimilliki vyema jukwaa baada ya kuutendea haki wimbo wa ‘Here I Stand’ wa Usher.  Kutokana na kulitawala vyema jukwaa mashabiki walishindwa kujizuia hivyo wakaenda nae sambamba katika kuimba huku wakimshangilia na kuonesha kuwa hawana upinzani na uimbaji wake. Majaji nao hawakuwa na lakuongeza zaidi ya kumpongeza huku jaji Hermes akimpongeza kwa kumwambia kuwa Tanzania inajivunia uwepo wake katika mashindano haya. Pia mwalimu wa washiriki wa Tusker Project Fame Musyoka alimpogeza sana kwa kuyazingatia yale yote aliyofundishwa na kumtaka akaze kamba.

Wasanii wengine waliopagawisha ni pamoja na Bior mshiriki kutoka Sudani ya kusini ambae anapendwa sana na mashabiki na anaweza kulimili jukwaa vilivyo japo alikuwa katika hatari ya kutolewa na badae kujikomboa. Pia msanii Patrick aliyingia jukwaani na kibao cha I’m an African in New York’ cha  Sting alionekana kuwabamba sana mashabiki na majaji hivyo kujihakikishia nafasi nzuri katika shindano hilo.

Mwisho wasanii wote walirudi jukwaani kwa pamoja ili kuvuna walichokipanda. Baada ya maelezo mafupi Jennifer alikuwa ni mshiriki wa kwanza kuchaguliwa kuwa katika hatari ya kutolewa huku ikiwa ni mara yake ya pili sasa kuwa katika hatari hiyo baada ya kunusurika katika kipindi kilichopita kwa kuokolewa na washiriki wenzake.  Wa pili katika hatari hiyo alikuwa Angel mshiriki kutoka Tanzania ambae anahitaji sana kura zetu watanzania ili kuendelea kubaki katika mashinano hayo kwani uwezo wa kuimba anao. Wa tatu alikuwa ni Phionah kutoka Rwanda na wa mwisho alikuwa ni Fessy  ambaye pia alirudi katika hatari kwa mara ya pili sasa.

Kabla ya onesho kuisha Dr Mich alimtambulisha mkurugenzi mpya wa muziki kwa wiki hii ambae ni jaji Hermes Bariki.

Meneja wa bia ya Tusker Sialouise Shayo kutoka katika kampuni ya bia ya Serengeti aliwashukuru sana na kuwapongeza washiriki Hisia na Angel kwa kuendelea kuiwakilisha vyema nchi yetu. Pia alisisitiza sana katika suala la kumpigia kura kwa wingi Angel kwani ana kipaji kikubwa na anaweza kusonga mbele kikubwa ni ushirikiano wa Watanzania katika kumuinua. Pia aliongeza kuwa kampuni hiyo ipo pamoja na watanzania katika kuhakikisha wanatuletea ushindi wa msimu huu.

Mpigie kura mshiriki Angel (Tusker 14) kutoka Tanzania ili aendelee kupeperusha bendere ya nchi yetu ili kumuwezesha kubakia katika shindano hilo. Usikose kufatilia moja kwa moja kipindi cha Tusker Project Fame msimu wa sita kupitia  televisheni za EATV saa 2:00 usiku siku ya Juma mosi na saa 1:30 usiku siku ya Jumapili,  pamoja na televisheni ya ITV  kuanzia saa 4:00 usiku Juma mosi na Jumapili.


Kunywa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako, haiuzwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.

0 comments: