Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Wednesday, October 23, 2013

MAENDELEO YA KILIMO TANZANIA-WAWEKEZAJI WAKUMBUSHWA- HAKUNA VIZUIZI


 Sikiliza Tone Radio Tz : http://www.toneradiotz.com/listenlive.php

Waziri__Chiza_akihutubia_ukumbi_wa_Reform_Club_London-pic_by_Urban_Pulse_4f920.jpg
Waziri Chiza akihutubia ukumbi wa Reform Club London
Bi_Rachel_Turner_wa_shirika_la_Maendeleo_DFID_Uingereza_akihutubia_88340.jpg
Bi Rachel Turner wa shirika la Maendeleo DFID Uingereza akihutubia
Waziri_Chiza_akiwa_na_Balozi_Kallaghe_mkutanoni_e514a.jpg
Waziri Chiza akiwa na Balozi Kallaghe mkutanoni
MP_Henry_Bellingham_chairs_meeting-pic_by_Urban_Pulse_b0950.jpg
MP Henry Bellingham chairs meeting
Balozi_Mhe_Peter_Kallaghe_akihutubia_mkutano_9b784.jpg
Balozi Mhe Peter Kallaghe akihutubia mkutano
Imeandaliwa kwa ushirikiano wa Urban Pulse na Freddy Macha
Wawekezaji wamehimizwa kutosikiliza propaganda za uongo kuhusu uporaji ardhi Tanzania na kuendeleza miradi ya kilimo nchini. Akiongea katika mkutano wa wafanyabiashara na viongozi wa taasisi, mashirika na makampuni mbalimbali ya ukulima na mazao Uingereza na Tanzania, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza alisisitiza serikali iko tayari kumsaidia yeyote anayetaka kuchangia idara hii muhimu ya uchumi.
Waziri Chiza aliyewasili London Jumatatu, kwa ziara ya kiserikali ya siku tano akiongoza msafara wa wanataaluma wa kilimo, alikuwa akijibu swali lililoulizwa mara kadhaa kuhusu ugawaji ardhi Tanzania.
Alifafanua: " Lipo gazeti moja lilisema serikali imechukua hekta milioni tatu. Si kweli. Ardhi iliyoshakaguliwa katika miaka miwili iliyopita si zaidi ya hekta 4,000. Habari hizi zimesababisha Tanzania kuondolewa katika kundi la nchi za kuwekeza kilimo. Hata wafanyakazi wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanatangaza uongo huu ambao ni marudio tu ya mambo yasiyo kweli yaliyoshazushwa zamani. Tafadhali njooni muongee na sisi wizarani na serikalini au taasisi zinazoaminika kama SAGCOT. Tutawaambia ukweli na kufanya nanyi kazi."
Mkutano husika ulifanyika ukumbi wa Reform Club mtaa wa Pall Mall, London, na kuhusisha wafanyabiashara wenye shughuli za kilimo Tanzania, makampuni makubwa yanayojishughulisha bara Asia, Afrika na Uingereza, mathalan duka maarufu la Sainsburys.
Kati ya wazungumzaji wakuu alikuwa Balozi wetu, Uingereza, Mhe Peter Kallaghe aliyesisitiza sera ya Tanzania kuendeleza mahusiano ya kibiashara badala ya kutegemea sana misaada ya kigeni; Rachel Turner mkurugenzi wa tawi la Mashariki na Afrika ya kati, idara ya serikali ya Uingereza ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID); Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha mpango maalum wa uendelezaji kilimo ukanda wa Kusini Tanzania ( SAGCOT), Geoffrey Kirenga na Profesa Peter Mahamudu Msolla, Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge ya Kilimo, Mifugo na Maji.
Katika hotuba yake Waziri Chiza alifafanua malengo matatu muhimu kuhusu ziara hii, yaani kuendeleza fursa ya kibiashara na uwezekaji, kujifunza teknolojia zinazohitajika na kuwaeleza wakulima na wafanyabiashara mambo takikana.
Msisitizo wa uwekezaji kupitia sekta binafsi ulitolewa mfano mzuri na Bwana Carter Coleman, Afisa Mtendaji wa Agrica linaloongoza mradi wa kuendeleza hifadhi, misitu na kilimo bora Afrika Mashariki.
Coleman ambaye amekuwa na mahusiano ya karibu na Tanzania toka 1987 alieleza baadhi ya shida zinazokabili kilimo kwa kusisitiza kuwa " kilimo Afrika ni aghali kuliko sehemu nyingine zote duniani."
Alitaja baadhi ya matatizo makuu kuwa kupatikana kwa umeme, ghala na hifadhi za mazao, matengenezo ya vifaa kama trekta, maradhi ya mimea na kujua mbegu zipi zitumike wapi na vipi.
"Kutokana na hayo kitengo cha uwekezaji na biashara ya binafsi ni muhimu sana kuendeleza kilimo Afrika," alikumbusha.
Mheshimiwa Waziri Chiza anatazamiwa kukutana na Watanzania leo Jumatano katika ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania London, uliomtayarishaji mkuu wa safari hii nzima.

0 comments: