Jumuiya za Watanzania Italy,kwa pamoja walifanya mkutano mkuu wa kihistoria siku ya jumamosi tarehe 8/2/2014.
Mkutano huo uliofanyika mjini Napoli,ulikuwa na madhumuni matatu makubwa. kwanza kuimarisha mshikamano baina ya Jumuiya za Watanzania nchini Italy, na pili kuzungumzia kero na matatizo ya Watanzania wanaoishi Italy.Wajumbe walichangia yote yaliyokusanywa katika mikutano na vikao vya awali.
Yote yaliyojadiliwa yatafanyiwa kazi na kufikishwa kunakostahili kwa ufumbuzi wa kudumu.
Jambo kubwa la tatu, Wajumbe waliunda kamati ya pamoja ya diaspora yenye wajumbe kutoka NAPOLI,ROMA,MODENA,GENOVA NA PADOVA. Na kuweka majukumu. Wajumbe pia walimchagua:
Ndugu Kagutta N.Maulidi (Mwenyekiti)
Ndugu Ricky JG.Bondo ( kaimu m/kiti)
Ndugu Andrew Chole Mhela (katibu)
Ndugu Mwinyimwaka Sarai (kaimu/katibu),
Ndugu LIlian Luhende (hazina)
Ndugu Abdulrahaman A.Alli (mjumbe)
Ndugu Erasmus Luhoyo (Mjumbe)
Ndugu Livinus Mwereke (Mjumbe)
Ndugu Awadhi Sulaiman (Mjumbe)
Ndugu Judith Joseph (Mjumbe)
Ndugu Zacharia Madjid Mhessa (Mjumbe)
Wajumbe wa mkutano wamependekeza kuwa baada ya kipindi cha miaka miwili utafanyika mkutano wa kutathmini utendaji wa kamati kwa ujumla.
Mwisho mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italy mh Abdulrahaman A.Alli aliwapongeza baadhi ya viongozi na wajumbe kwa kuwatunukia shahada za uongozi bora na uhadilifu.
Pichani Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italia Mh Abdulrahaman A.Alli(aliyeshika cheti) akimtunukia cheti cha uadilifu na uongozi bora Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma Mh. Andrew Chole Mhela. |
Mwenyekiti wa kamati ya Diaspora Mh Kagutta N.Maulidi akionyesha cheti alichotunukiwa na mh Mwenyekiti kwa uadilifu na uongozi bora wa jumuiya ya Watanzania Italy . |
Wajumbe wakifuatilia mkutano kwa makini |
viongozi katika picha ya pamoja |
hii ndio kamati ya Diaspora |
Mwenyekiti wa kamati ya Diaspora katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati. |
Kaimu Mwenyekiti wa Diaspora Mh Ricky JG.Bondo akifafanua jambo kwa mjumbe ndugu Mohamed Mnondwa, baada ya kikao. |