Msanii aliyetamba enzi hizo kwa umahili wake wa kuchea na nyoka Salma Moshi akisalimiana na kumkabidhi picha za baadhi ya kazi ya sanaa hiyo aliyofanya enzi hizo Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula alipokwenda kujitambulisha rasmi kwenye Ubalozini wa Tanzania uliopo Washington, DC siku ya Jumanne Feb 18, 2014.
Msanii wa siku nyingi na mahili wa kucheza na nyoka Bi. Salma Moshi aliongea na Mhe. Balozi Libetara Mulamula alipotembelea Ubalozi wa Tanzania Washington, DC siku ya Jumanne Feb 18, 2014
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tamzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula akimsikiliza msanii wa siku nyingi, Bi Salma Moshi (hayupo pichani) alipotembelea Ubalozi wa Tanzania Washington, DC siku ya Jumanne Feb 18, 2014.
Afisa Mgendi Nzowa akiwa kwenye mkutano huo.
Afisa Suleiman Saleh akijumuika pamoja na Balozi kwenye mkutano huo.
mama Salima alisema MAPROMOTA wengi baada ya kupata wamekuwa wanawatelekeza wasanii na pato kubwa linaenda kwao bili kunufaisha msanii na hata wale wanaobahatika kuja kupiga nje wamekuwa wanaishia kuwapigia watanzania ifike wakati wakija huku waweze kutumbuiza na wenyeji wa huku alitoa mfano kama JZ aende Tanzania halafu awapigie waMEREKANI mama Salima alikemea vikali swala la kukopi kazi za sanaa linarudusha nyuma maendeleo ya wasanii na aliomba SERIKALI kutoa adhabu kali kwa watakao bainika na kusimamia swala la hakimiliki mama salima alisema imefika wakati sasa wasanii kuwa na WANASHERIA hii itasaidia kulinda haki zao Mama salima alimshuru sana MH RAIS amekuwa wakati wote karibu na wasaniina hata hivi karibunialiwaalika kwenye chakula hivyo naomba wasanii tuitumie nafasi hiyo
Alisema kuhusu tunzo ziwe zinatoa kwa wasanii wa sanaa za maonyesho na wakati umefika kutoa kibali kwa waandaaji wengine si vibaya zikawa zaidi ya moja pia aliombakusaidia kujenga maktaba kwenye eneo la viwanja vya wasanii MKURANGA na kumpongeza mwenyekiti wa wasanii bw TWALIBU
MH BALOZI alimshukuru sana msanii huyo na kumpongeza kwa kazi nzuri ya kuwakilisha nchi na kuwa msanii atakayekuwa mfano kwa wengine alisema kuhusu Hakimiliki SERIKALI imejizatiti kikamilifu kuhakikisha haki za msanii zinalindwa alisema ni vyema wasanii wakajua haki zao hii itawasaidia sana aliongolea MAPROMOTA ni vyema kuangalia maslahi ya wasaniikwanza MH Balozi alisifu sana kazi zinazofanywa na wasanii mbalimbali nchinina kuitangaza NCHI yetu
0 comments:
Post a Comment