Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania unakutaarifu Harambee ya kukusanya pesa
kwaajili ya kusaidia kuandaa semina ya kuwaelimisha Wabunge wa Bunge la
katiba umuhimu wa raia pacha kama wewe ni mkereketwa wa hili swala na
usiku haulali linakufulukuta na hii ni kwa faida yako na vizazi vyetu
vijavyo hata kama wewe hautalifaidi, kufika kwako kwenye harambee hii
utakuwa umewajengea watoto wako msingi mzuri wa DUAL CITIZENSHIP.
Hii ni haki yako lazima upiganie hata kama watu wengine hawaoni umuhimu
wake ni kwa sababu ya kutoelewa na kujisahau hata kama utajichubua
ufanane na mzungu asili yako itabaki Mtanzania, wewe umezaliwa Tanzania,
umekulia Tanzania, umesomea Tanzania ni Mtanzania halisi kwa nini uwe
mgeni kwa nchi ya watu wakati una nchi yako Tanzania?
Fikiri kwa makini uraia uliopewa na nchi nyingine ni wa makaratasi tu
siku wakikunyang'anya utaenda wapi wakati nchi yako ulikozaliwa
inakukataa kwa sababu ya hilo karatasi ulilopewa kwa ajili ya maisha ya
ughaibuni yawe nafuu. kumbuka ughaibuni sio nchi yako, Tanzania ndiko
ulikozaliwa daima utaipenda Tanzania na siku zote utabaki kuwa Mtanzania
asilia.
Harambee itafanyika kesho Jumapili March 23, 2014 Meadowbrook park address ni 7901 Meadowbrook lane, Chavy Chase, MD 20815
Jumiya DMV itachoma nyama huku tukifanya harambee
Ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzio.
MIMI NI MTANZANIA, NIMEZALIWA TANZANIA, NIMEKUILIA TANZANIA, NAISHI
UGHAIBUNI NDIO MAANA NASEMA URAIA PACHA NI HALALI YANGU NA HAKI YANGU YA
MSINGI.
0 comments:
Post a Comment