Berlin, Ujerumani
Mchekeshaji
maarufu kutoka nchini Tanzania Muarabu wa Dubai a.ka Mpoki ameondoka
nchini Ujerumani kurudi nyumbani Tanzania baada ya ziara yake ya siku 4
kukamilika. Msanii huyo ambaye alifanya ziara nchini ujerumani baada ya
kualikwa na Umoja wa wa Watanzania Ujerumani (U T U) kwa ajili ya
Sherehe za muungano wa Tanzania, zilizoambatana na kongamano la
kibiashara pamoja na Mkutano mkuu wa uchaguzi wa
U T U.
Mchekeshaji
huyo maarufu kutoka kundi la Orijino Komedi aliweza kuburudisha
waliohudhuria katika sherehe hizo kubwa na za aina yake katika jiji La
Berlin Ujerumani.
Kufuatia
uchaguzi mkuu wa U T U. Bw. Mfundo Peter Mfundo amepata ushindi
mkubwa wa % 98 na kuendelea kuwa Mwenyekiti wa U T U kwa kipindi kingine
cha miaka 2.
Nafasi
ya makamo Mwenyekiti ilinyakuliwa na Bw. Peter Kazaura nafasi ya
Katibu imechukuliwa na Bi. LiLian Sorogo, nafasi ya Muweka hazina
imechukuliwa na Rajab Kaoneka.
Wajumbe
wa kamati ni. Zenat Jamal, Dr. Andreas Wesselmann, Julius Tsaxarra,
Joyce Rupia, Vital kazimoto, na Fulgens Kisalya. Mutano huu wa Uchaguzi
ulihudhuriwa na Mgeni Rasmi Mh. Naibu Balozi wa Tanzania nchini
ujerumani Bw. Mvulla. Mwenyekiti
wa U T U Bw Mfundo Peter amesema timu yake mpya inategemea kubadilisha
sura nzima na mwenendo wa Umoja huu, ndani ya kipindi cha miezi 6 ya
uongozi mpya. Chanzo cha habari kilinyetisha.
Baada
ya mkutano wa uchaguzi kumalizika mnamo saa 11:30 alasiri, Viongozi wa
U T U na Wanachama walijumuika na watanzania wengine katika tafrija ya
chakula cha jioni katika Hotel ya MARITIM HOTEL Berlin. ambayo
iliandaliwa rasmi na Ubalozi wa Tanzania nchini ujerumani ili
kuhitimisha sherehe za Muungano wa Tanzania katika Tafrija hiyo kubwa
walihudhuria wageni mbali mbali, Diplomats, na burudani mbali mbali
zilikuwepo zikiwemo ngoma za asili kutoka Tanzania na Vichekesho kutoka
kwa Mchekeshaji MPOKI, pia kulikuwa na Muziki wa kunesanesa. Msanii wa
Movie na mtayarishaji wa kipindi cha Beyond the Borders bi Devota
Alfred aliweza kufanya mahojiano na wasanii pamoja na viongozi
waliohudhuria sherehe hizi. naye mtangazaji wa Deutsche welle idhaa ya
kiswahili Bw Sudi Mnete hakuwa mbali siku hii akirepoti kutoka katika
eneo la tukio.
0 comments:
Post a Comment