Betty Boniface
Nelly Kamwelu
Warembo
wawili wa waliowahi kushinda taji la Miss Universe, Nelly Kamwelu na
Betty Boniface leo (Jumamosi) watapanda jukwaani mjini Moscow, Urusi
kushiriki katika maonyesho ya mavazi ya kuadhimisha miaka 50 ya Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar.
Warembo
hao waliondoja nchini juzi na tayari wapo mjini Moscow kwa ajili ya
maonyesho hayo ambayo pia yatashirikisha waonyesha mavazi mbali mbali wa
Tanzania.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai alisema jana
kuwa warembo wake wamepata heshima hiyo kutokana na ukweli kuwa Miss
Universe imefanya kazi kubwa sana ya kuitangaza nchi kimataifa na hasa
mwaka jana baada ya mrembo wake, Betty Boniface kufanya vyema mjini
Moscow.
Alisema
kuwa katika mashindano ya mwaka jana, Betty aliweza kuitangaza nchi
vilivyo pamoja na kufanyiwa mahojiano makubwa na vyombo vya habari mbali
mbali vya kimataifa na kuitangaza nchi ikiwa pamoja na sekta ya
Utalii.
“Hii
ni heshima kubwa ambayo Watanzania inadidi tujivunie, warembo wetu
wamepata fursa hiyo kubwa ya kuonyesha maonyesho ya mavazi
yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, ni nafasi pekee
ambayo tumepewa na tunashukuru kuitumia fursa hiyo,” alisema Maria.
Aliongeza
kuwa hatua hiyo imewapa hamasa zaidi na kujua umuhimu wa mashindano
hayo hasa kwa kufanya vyema katika mashindano mbali mbali. Mwaka 2007,
mrembo wa kwanza wa Miss Universe Tanzania, Flaviana Matata alimaliza
katika hatua ya tano bora nchini Mexico na kuipaisha nchi. Flaviana kwa
sasa anafanya kazi nchini Marekani na ni mmoja wa waonyesha mitindo wa
kimataifa.
0 comments:
Post a Comment