Robert Otto
Mtangazaji AJ
Na Vijimambo Blog
Na Vijimambo Blog
Robert Otto kabla ya kuja Marekani aliendesha maisha na alipata elimu yake ya msingi ikiwemo elimu ya sekondari Dar es Salaam katika shule ya Azania na Tambaza na aliishi Keko juu na mwaka 1997 alifika nchini Marekani na alianzia maisha yake Brooklyn, New York na baadae akahamia Springfield, New Jersey na mwaka 1998 alihamia Wichita jimbo la Kansas na kujiunga na chuo cha Wichita State na kusomea computer engineering, electrical engineering, mathematics statistics na Nursing na alifuvu masomo yake 2005 na kubahatika kupata bachelor degree ya masomo yote na kuwa Best Student kwenye chuo hicho cha Wichita State.
Robert Otto alipomaliza masomo yake ya Nursing alihamia Kansas City, Kansas mwaka 2007 na kuanzisha kampuni yake ya Home Health Care na baadae kufungua vyuo vya Nursing vijulikanavyo kama Kansas College of Nursing- Lenexa na Kansas College of Nursing-Manhattan.
Robert Otto aliwaasa Watanzania wenzake wanaokwenda Ughaibuni kutafuta maisha walipe kipaumbele swala la elimu kwani kuna usemi ulisema "elimu ni ufunguo wa maisha" aliongezea kwa kusema yeye amesoma masomo mengi ni kwa sababu hakujua ni nini anachotaka kufanya japo sasa amejikita kwenye maswla ya Nursing na masomo mengine ameyaweka kama akiba na sababu ya kufanya hivyo aiangalia kama kimoja wapo kikienda kombo haitaji tena kurudi shule yeye ataendelea na kitu kingine.
Robert Otto anafikiria kufungua maswala ya Health Care nyumbani Tanzania siku zijazo na swala la raia pacha amesema haelewi kwanini Tanzania inakigugumizi kuhusiana na swala hili swala hili lipo wazi na faida zake zipo wazi na nchini zilizokubali kuhusu raia pacha zimenufaika sana akitoa mfano wa mcheaji Didier Drogba ambaye ni raia wa Ufaransa lakini amepata nafasi ya kuchezea Ivory Coast na hiyo ni faida moja wapo zipo nyingi sana. Kwa hiyo naiomba Tanzania kuliangalia swala hili kwa upana na upeo mkubwa na wasifikirie kizazi chetu tu kuna vizazi na vizazi yote ni kwa faida ya nchi yetu Tanzania.
0 comments:
Post a Comment