Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Thursday, April 3, 2014

SOMA HII: MABINTI MSIDANGANYIKE NA MAISHA YA HUKO CHINA, ACHENI TAMAA.


To be honest hali ni mbaya sana kwa baadhi ya mabinti wakitanzania nchini China to be specific huko MACAU. Inabidii Serikali ingilie kati hawa mabinti walioko huko warudi nyumbani. Jamani kama una ndugu yako huko MACAU please mtafute njia yeyote muwasaidie na mimi pamoja na watu wangu tunajaribu kusaidia kwa hali yeyote ile ili warudi nyumbani. Naskia ni mabinti wengi sana wako huko na wamekwama. 

Kilicho niskitisha zaidi ni baada ya mimi kupost zile clip hao mabinti walivamiwa huko wanako ishi na kupigwa sana, kunyanganywa kila kitu na kutishiwa kuuwawa. 

Ushauri wangu na wito kwa nyie watoto wa kike mnao taka maisha rahisi ukweli ni kwamba hakuna maisha rahisi na matokeo yako ndo kama haya yanayo wapata wenzenu huko China. 

Hii issue si uongo ni kweli kabisa. Sasa msidanganyike eti mnapelekwa China kutafutiwa kazi kataa kabisa kazi mnayo pelekwa kufanya ni kujiuza miili yenu na pesa zote wana chukua hao wanao jiita MAMA au BOSS LADY na passport yako wanaichukua unafanywa mtumwa wao na ukikataa wana kutumia wanigeria wakupige au kukufanyia kitu kibaya kama yule mmoja aliye uwawa na kutolewa figo lake maana viungo navyo vinasoko sana huko China. 

Jamani tusaidiane kuwaelimisha hawa mabinti. Huko China hakufai kama huna hela yako yakukupeleka huko bora ubakie tu nyumbani Tanzania ufe na umaskini wako. Hizo picha mnazo ona huko Instagram na humu facebook nyingi ni za kuwachuuza na ni fake life za watu. Ridhika na ulicho nacho.

So far kwa kushirkiana na team yangu tumefanikiwa kumuokoa binti mmoja na yuko njiani kuelekea nyumbani Tanzania. Process za kusaidia wengine zinaendelea.

Tunaomba ualozi wa Tanzania China usilifumbie macho suala hili maana kitanzania tunafundishwa kwamba mtoto wa mwenzako ni wako pia. Kazi yenu ni nini kama mnashindwa kusilikiza vilio vya hawa mabinti? 
 
NA JESTINA GEORGE BLOG.

0 comments: