Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake
Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron alipomtembelea ofisini kwake
10 Downing Street jijini London kwa mazungumzo Machi 31, 2014.
Uingereza
inajivunia kuwa nchi inayoongoza katika uwekezaji nchini Tanzania na
itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kiuchumi na kuleta
maendeleo .
Waziri
Mkuu wa Uingereza David Cameron amemuambia Rais Kikwete wakati wa
mazungumzo yaliyofanyika 10 Downing Street, Leo tarehe 31 March, 14,
ambapo ndipo yalipo Makao Makuu ya Waziri Mkuu wa Uingereza.
“Tunafurahia sana uhusiano wetu na kujivunia kuwa tunaongoza katika
Uwekezaji nchini Tanzania” Bw. Cameron amesema na kumhakikishia Rais Kikwete kuwa Uingereza iko tayari kutoa misaada zaidi.
“Tunafurahia sana uhusiano wetu na kujivunia kuwa tunaongoza katika
Uwekezaji nchini Tanzania” Bw. Cameron amesema na kumhakikishia Rais Kikwete kuwa Uingereza iko tayari kutoa misaada zaidi.
Rais
Kikwete amewasili nchini Uingereza tarehe 30 Machi, 2014 kwa ajili ya
ziara ya kikazi ya siku 3 kufuatia mualiko wa Bw. Cameroon ambaye pia
amemuomba Rais Kikwete aendelee kutoa mchango wake wa mawazo katika
masuala ya kimataifa hasa baada ya mwisho wa muda wa malengo ya
millennium ya 2015.
“Tunakaribia
mwisho wa muda wa malengo ya millennia Mwaka 2015, tutahitaji kuweka
vipaumbele vingine baada ya hivyo kama kuondosha umaskini, Maji safi na
salama, masuala ya ufisadi na utawala bora, natumaini utaendelea kutoa
mchango wako baada ya malengo hayo kufikia tamati” Waziri Mkuu Cameron amemuambia Rais Kikwete ambapo Rais amekubali ombi hilo na kuahidi ushirikiano wake.
Mapema leo
asubuhi Rais amekutana na mtoto wa Mfalme Prince Andrew katika makazi
ya Malkia ya Buckingham ambapo wamebadilishana mawazo kuhusu mambo
mbalimbali ya Kimataifa na Kijamii.
Kabla ya
kwenda Buckingham Rais amefungua mkutano kuhusu uwekezaji na kuelezea
fursa na nafasi zilizopo za uwekezaji nchini Tanzania na kuelezea
kwanini wawekezaji watakuwa wanafanya uamuzi bora kwa kuwekeza Tanzania
kuwa ni pamoja na;
“Fursa nyingi, amani, usalama, soko la kutosha na kubwa kwa vile Tanzania iko katika Umoja wa Afrika Mashariki, Ukanda wa Maziwa Makuu na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika,hivyo kuwa na uhakika wa soko kubwa na pana” amesema.
“Fursa nyingi, amani, usalama, soko la kutosha na kubwa kwa vile Tanzania iko katika Umoja wa Afrika Mashariki, Ukanda wa Maziwa Makuu na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika,hivyo kuwa na uhakika wa soko kubwa na pana” amesema.
Katika
ziara yake Rais pia amekutana na Mstahiki Meya wa Jiji la London Mama
Alderman Fiona Woolf na kukaribishwa rasmi Jijini London. Mstahiki Meya
anatarajia kutembelea Tanzania, Mwezi Septemba Mwaka huu.
Rais
alipowasili London tarehe 30 Machi,2014, alikutana na Watanzania
wanaoishi nchini Uingereza na kuwaeleza maendeleo yaliyopo nchini
Tanzania.
Rais anaendelea na ziara yake nchini Uingereza.
0 comments:
Post a Comment