Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Thursday, November 6, 2014

UCHAGUZI WA VIONGOZI UMOJA WA WATANZANIA NORTH CAROLINA UTNC 2014, ANNA SIMTAJI MMANYWA NDIYE MWENYEKITI MPYA


Uchaguzi wa viongozi uliofanyika Jumamosi Novemba 1, 2014 na kuwachagua viongozi wapya wa jumuiya ya Watanzania North Carolina ambako aliyekua mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Geofrey Lipana alimaliza muda wake na kumkabidhi kiti Anna Simtaji Mmanywa ambaye atasaidiana na viongozi wenzake waliochaguliwa. Katika uchaguzi huo,  kura zilipigwa kwa wazi na kuandika historia mpya kwenye jimbo hilo la North Carolina. 

Mbali na Anna Simtaji Mmanywa viongozi wengine waliochaguliwa ni Katibu ni Mshobozi Kamugisha, Katibu msaidizi ni Mariam Kalala Nyang'oro, Mweka hazina ni Glory Alex na Mweka hazina msaidizi ni Niwagila Kamugisha. Wajumbe wa bodi ni Agnetti Kamugisha, Zainab Black, Lilian Kimweri Danieli, Esther Idassi na Dkt. Yusuf.
Wanajumuiya wa North Carolina wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kufanyika uchaguzi wa viongozi wao uliofanyika siku ya Jumamosi Novemba 1, 2014 Durham, North Carolina nchini Marekani.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Bwn. Geofrey Lipana akitoa shukran na nasaha zake katika uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ya Watanzania NC uliofanyika siku ya Jumamosi Novemba 1, 2014 Durham North Carolina nchini Marekani.
 Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Watanzania North Carolinaaliyechaguliwa Anna Simtaji Mmanywa akijinadi kwa wapiga kura wake siku ya uchaguzi wa Jumuiya ya UNTC uliofanyika siku ya Jumamosi Novemba 1, 2014 Durham, North Carolina.
Mweka hazina aliyechaguliwa Bi. Glory Alex akijieleza mbele ya wapiga kura wake katika uchaguzi wa viongozi wa jumuiya ya Watanzania North Carolina uliofanyika siku ya Jumamosi Novemba 1, 2014 Durham.
Mjumbe wa bodi Dkt. Yusuf na mama mwenye nyumba yake walipokuwa kwenye uchaguzi wa jumuiya ya Watanzania NC siku ya Jumamosi Novemba 1, 2014.
 Mwenyekiti mstaafu Bwn. Nassoro Basalama akichangia jambo siku ya uchaguzi wa viongozi UNTC uliofanyika Jumamosi Novemba 1, 2014 Durham, North Carolina nchini Marekani.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Niwagila Kamugisha na mama mwenye nyumba yake wakiwa tayari kutumia haki yao ya msingi ya kuwachagua viongozi wapya kwenye uchaguzi wa viongozi wa UTNC uliofanyika siku ya Jumamosi Novemba 1, 2014 Durham, North Carolina nchini Marekani.
 Pendo Nyang'oro na mama mwenye nyumba wake Bi. Mariam wakiwa pamoja na Aunty Esther (kulia) wakiwa makini huku wakifuatilia uchaguzi kwa karibu.
 Saburi (kushoto( akijadii jambo na Eliud siku ya uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ya Watanzania UNTC siku ya Jumamosi Novemba 1, 2014 Durham, North Carolina nchini Marekani.
 Wanajumuiya wa North Carolina wakifuatilia uchaguzi wa viongozi wao.
Wanajumuiya wakipiga kura ambazo zilikuwa za wazi za kuwachagua viongozi wao. 
kuotoka kushoto ni Joyce, Flora na Zainab ndani ya uchaguz
Kamati ya uchaguzi kutoka kushoto ni Uncle Sichele, Tausi na Teddy
Katibu mpya wa UTNC aliyechaguliwa Mshobozi Kamugisha.

Picha na Lucas Mmanywa mwakilishi wa Vijimambo Winston Salem, NC.

0 comments: