Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Monday, December 8, 2014

DICOTA WAMKABIDHI BALOZI LIBERATA MULAMULA RIPOTI YAO YA DICOTA CONVENTION 2014 ILIYOFANYIKA NORTH CAROLINA

Viongozi wa DICOTA Lunda Asmani na Dr. Kurwa Nyigu walifika jioni ya Desemba 8, 2014 ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington DC kumkabidhi Mhe. Liberata Mulamula ripoti ya mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2014 uliofanyika mapema mwezi Oktoka kati ya tarehe 2 mpaka 5.

Katika makabidhiano hayo yaliyo ambayo yalikua ni maelezo ya viongozi wa DICOTA na maoni ya wahudhuriaji wa mkutano huo wa kongamono wa ndani na nje ya Marekani ikiwemo DVD 2 ya mkutano huo.

Viongozi hao walimweleza Mhe. Balozi Liberata Mulamula kwamba mkutano wa DICOTA COnvention 2014 ulikua wa mafanikio na kutokana na swala la uchaguzi mkuu mwaka 2015 mkutano wa kongamano wa DICOTA hautafanyika na matarajio yao ni kuufanya mwaka 2016 mji na jimbo bado haijajulikana. Pia bwn. Lunda Asmani alielezea DICOTA inavyojihusisha kwa karibu na viongozi wa Jumuiya za Watanzania wa majimbo nchini Marekani huku wakijaribu kuboresha mahusiano na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ambao hapo nyuma ulilegalega.

Mhe. Balozi Liberata Mulamula alianza kwa kuwashukuru viongozi hao kwa kupata wasaa wa kufika Ubalozini na kukabidhi ripoti na DVD na kusema alifurahi sana na mkutano wa DICOTA uliofanyika Durham, North Carolina kwani ulikua wa mafanikio  makubwa na ulitoa fulsa nyingi kwa wahudhuriaji wa mkutano huo mwaka huu. Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliwaasa viongozi wa DICOTA kuendelea kuwasiliana na wadhamini wa mkutano huo hasa walioweza kufika na kunadi bidhaa zao ili waweze kujua maendeleo ya bidhaa walizonadi kwenye mkutano huo akitolea mfano wa Azania Bank, NHC, PPF na wengine ambao wangependa kujua ni Watanzania wangapi nchini Marekani walionufaika na ujio wao kwenye mkutano huo. Kwa kufanya hivyo kunaleta mahusiano mazuri na wadhamini ili wasiishie hapo wazidi kuwatangza na wao kujitangaza kupitia mikutano ya DICOTA.

Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliendelea kwa kusisitizia viongozi hao kuendeleza mahusiano na Jumuiya za Watanzania nchini Marekani hususani viongozi wa Jumuiya hizo na kutafuta uwezekano wa kukutana nao mara kwa mara na akashauri Jumuiya zinapofanya mijumuiko yao na vyema na wao wakatuma mwakilishi kuhudhuria mijumuiko hiyo huku akitoa mfano wa sherehe za Uhuru zinafanyika kwenye majimbo toafauti ni vizuri DICOTA kutuma mwakilishi ili kuwa karibu na Jumuiya hizo pia kutajenga mshikamano wa karibu na Viongozi wa Jumuiya hizo.

Mwisho viongozi wa DICOTA waliuomba Ubalozi wasisite kuwaita mara wanapohitaji msaada wao kwani wanapotoa msaada kwa Ubalozi hujisikia kufarijika kwani ni furaha ni kutumia utaalamu na uzowefu wao katika kusaidia kusukuma kurudumu la maendeleo kwa kwa pamoja tunaweza.

 Viongozi wa DICOTA Lunda Asmani (kushoto)na Dr. Kurwa Nyigu wakitia saini kitabu cha wageni mara tu walipofika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington, DC kuonana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamuala (hayupo pichani) na kumkabidhi ripoti ya mkutano wa kongamano wa DICOTA uliofanyika mapema mwezi wa Oktoba kwenye tarehe 2 mpaka 5 2014.
 Viongozi wa DICOTA Dr. Kurwa Nyigu (kushoto na Lunda Asmani(wapili toka kushoto) wakifanya mkutano wa makabidhiano ya ripoti ya mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2014 na Mhe. Liberata Mulamula akiwemo Afisa Ubalozi Switebert Mkama(kulia) jioni ya Jumatatu Desemba 8, 2014 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo barabara ya 22 NW, Washington, DC.
 Mkutano wa makabidhiano ukiendelea
 Kiongozi wa DICOOTA Lunda Asmani akimkabidhi Mhe. Balozi Liberata Mulamula Ripoti ya mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2014 uliofanyika mapama mwezi wa Oktoba Durham, North Carolina nchini Marekani.
 Kiongozi wa DICOTA Lunda Asmani akitoa maelezo kwa Mhe. Balozi Liberata Mulamula kuhusiana na ripoti hiyo.
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiipitia kwa haraka haraka ripoti hiyo
 Kiongozi wa DICOTA Lunda Asmani akimkbidhi Mhe. Balozi Liberata Mulamula DVD za mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2014 uliofanyika mapema mwezi Oktoba Durham North Carolina nchini Marekani.
 Kiongozi wa DICOTA Lunda Asmani akiemwelezea jambo mhe. Balozi Liberata Mulamula.
 Kiongozi Lunda Asmani akiendelea kuelezea jambo huku kiongozi mwenzake Dr. Kurwa Nyigu akimsikiliza.
Afisa Ubalozi Switebert Mkama akifuatilia mkutano wa makabidhiano wa ripoti ya DICOTA Convention 2014 uliofanyika Durham, North Carolina mapema mwezi wa Oktoba 2014.

0 comments: