Zainab Buzohera Enzi ya Uhai Wake.
Sekunde dakika masaa siku wiki miezi
imepita na leo ni mwaka tangu ulipoitwa na Mwenyezi Mungu (S.W.T). na
kutuachia uchungu usioelezeka . Pengo ulilotuachia haliwezi kuzibika
bali tunamshukuru Mungu kwani kazi yake haina makosa. Tunaendelea
kumuomba akupumzishe kwa amani hadi hapo tutakapo kutana kwani sisi wote
ni wapitaji.unakumbukwa na baba mzee Haroun mama Bi Rehema wadogo zako
ndugu jamaa marafiki na wote waliokufahamu .unakumbukwa sana kwa ucheshi
wako moyo wako wa utoaji na ushirikiano na wengi . Mwenyezi Mungu
akupumzishe kwa amani na aendelee kutufariji . Sisi wote ni wake na
kwake tutarejea.Inna lillah wa inna lillah rajiun
0 comments:
Post a Comment