Ujumbe wa Serikali ya Tanzania
ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb)
katika mazungumzo na Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar bin Saud bin
Mohammad Al-Saud ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi
Arabia. Wengine katika picha kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya
Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Balozi wa Tanzania Saudi Arabia
Prof. Abdillah Omari; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na
Mazingira Mhe. James Lembeli; Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe.
Peter Msigwa; Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi;Mkurugenzi wa Idara
ya Wanyamapori Herman Keraryo na Afisa wa Ubalozi Ndg. Sufian.
Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) akisisitiza jambo katika mazungumzo na Mwana wa
Mfalme wa Saudia Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud ambaye pia ni
Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili
na Utalii Dk. Adelhem Meru (kati) akiongea katika mazungumzo baina ya
ujumbe wa Tanzania na Saudi Arabia. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli na kushoto ni Balozi wa
Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari.
Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince
Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya
Wanyamapori ya Saudi Arabia akiongea katika mazungumzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan
Kijazi akichangia jambo katika mazungumzo hayo. Wengine pichani kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Herman Keraryo; Waziri
Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa; Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli na Balozi wa
Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (wa tatu kushoto) ukiwa
katika picha ya pamoja na Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar (wa nne
kushoto) jijini Riyadh, Saudi Arabia. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa
Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari; Katibu Mkuu Wizara ya
Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii
Mhe. Peter Msigwa; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na
Mazingira Mhe. James Lembeli; Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi na
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Herman Keraryo.
Ujumbe wa Mwana wa Mfalme wa
Saudi Arabia ukifuatilia mazungumzo hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia) akiwa na mazungumzo na (kutoka kulia) Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Mwenyekiti wa Kamati
ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli na Waziri
Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa muda mfupi kabla ya kuanza
kwa mazungumzo baina ya Tanzania na Saudi Arabia jijini Riyadh, Saudi
Arabia.
0 comments:
Post a Comment