
Kundi hili limewahusisha vijana wenye taaluma mbalimbali kwa lengo la kurejea matatizo ya jamii na taifa lao la Tanzania, na kuangalia wajibu na uezo wao katika kushiriki kupigana na changamoto hizo.
Vijana hawa wakidai kuwa wamechoshwa na hulka ya waliowengi, kukaa pembeni na kulaumu serikali.
Akidai Admin wa kundi hili Bwana Nassor Basalama kuwa kazi ya kujenga nchi ni ya wananchi. Sasa ikiwa mwananchi ndio anayefanya kazi ya kulalamika, nani atakaye fanya kazi ya kujenga? Hii ni hulka ya kukosa miono naya kifukara ya kutafuta kujiridhisha kwa kutobeba majukumu mazito ya ujenzi wa taifa.
Kundi hili limewahusisha viongozi wa Jumuiya zote za watanzania marekani, na taasisi mbalimbali.
Wiki 2 zilizopita kundi hili lilikabidhi $3000 kwa NGO ya Albino charity na AFROBINO kwa lengo la kusaidia watanzania wanaoathirika kwa ugonjwa wa ngozi na macho. Pia kundi hili limeandaa powerpoint ambayo imeisambaza kwa jumuiya za watanzania na kwa ajili ya kuelimisha juu ya Albinism.
CHANZO BLOG YA VIJIMAMBO
0 comments:
Post a Comment