.jpg)
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akihojiwa na Priscilla Lecomte wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa. (Picha: UN/JosephMsami)
Rais
wa Tanzania Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa jopo la Umoja wa
Mataifa la kusaka jinsi dunia inaweza kukabiliana na magonjwa ya mlipuko
kwa siku za usoni, amesema leo kwamba anatarajia kutoa mapendekezo juu
ya mapugunfu yaliyoonekana wakati wa kupambana na Ebola.
Akihojiwa
na Priscilla Lecomte na Jospeh Msami wa idhaa hii, ameeleza kwamba
wanachama wa jopo hilo baada ya kuzungumza na wataalam wa afya mjini new
York, watatembelea Geneva, Uswisi, ili kujadiliana na wadau wa shirika
la afya ulimwenguni, WHO na mashirika mengine, halikadhalika watasafiri
kwenda nchi zilizoathirika na Ebola.
Hapa
Rais Kikwete anaanza kwa kuelezea jukumu la jopo hilo ambalo ripoti
yake ya awali wataiwasilisha mwezi Septemba, ripoti ya mwisho
ikitarajiwa mwisho wa mwaka .
KUSIKILIZA BONYEZA HAPA
0 comments:
Post a Comment