Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akiongozana na Mke wa Balozi wa India nchini Tanzania
Mheshimiwa Debnath Shaw wakielekea kwenye jengo la Makumbusho ya Indra Gandhi
huko New Delhi tarehe 18.6.2015. Mama Salma yupo nchini India akiambatana na
Rais Kikwete kwenye ziara siku 4 ya kiserikali kwa mwaliko wa serikali ya India.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitembelea
sehemu mbalimbali zilizohifadhiwa kumbukumbu za aliyekuwa Waziri Mkuu wa India
Marehemo Indra Gandhi wakati wa uhai wake. Marehemu Idra Gandhi aliuawa kwa
kupigwa risasi tarehe 31.10.1984 akiwa kwenye viwanja vya nyumba hiyo ambayo
alikuwa akiishi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini kwenye kitabu
cha kumbukumbu ya Marehemu Indra Gandhi wakati alipotembelea makumbusho ya
waziri mkuu huyo huko New De;lhi nchini India tarehe 18.6.2015
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akiagana na kiongozi anayesimamia Makumbusho ya aliyekuwa
Waziri Mkuu wa India Marehemu Indra Gandhi (jina lake halikuweza kupatikana)
mara baada ya kumaliza kutembelea makumbusho hayo tarehe 18.6.2015.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akipewa taarifa
mbalimbali na Bwana Rajan Madan,
Mkurugenzi wa Uzalishaji katika Kiwanda
cha New Holland Fiat Limited kuhusiana na utengenezaji wa matrekta kwenye
Kiwanda hicho huko New Delhi. Mama Salma
Kikwete aliambatana na Rais Kikwete kuzuru kiwandani hapo ili kujionea utengenezaji wa matrekta.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
0 comments:
Post a Comment