Taarifa
zinazosambaa kumhusu Mkuu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) Jenerali Davis
Mwamunyange zilizosambaa kwenye mitandao ya jamii kwamba amekula chakula
chenye sumu na amekimbizwa jijini Nairobi nchini Kenya kwa matibabu
hazina ukweli wowote.Ni uzushi.
Kwa
mujibu wa taarifa za familia ya Jenerali Mwamunyange pamoja na makao
makuu ya jeshi ambazo Globu ya Jamii imezisaka na kuzipata, kiongozi
huyu wa JWTZ hivi sasa yupo nchini Italia kwa ziara ya kikazi ya siku
tisa kama anavyoonekana pichani na hajambo kabisa na yu bukheri wa afya.
Hii
ni changamoto kwa wakala wa mawasiliano nchini (TCRA) ambayo imekuwa
ikilaumiwa kwa ukimya wake wa kutochukua hatua thabiti kuthibiti uongo
kama huu kwa kuwatafiti, kuwabaini na kuwachukulia hatua watu kama hawa
wenye nia ya kuleta taharuki na machafuko nchini.
Wananchi
wengie waliohojiwa na Globu ya Jamii wanahoji endapo kama kweli TCRA
ipo na kama ipo ina vifaa vya kisasa iliyodai wanavyo kuwabaini watu
kama hawa, na kwa nini hawajafanya kweli toka sheria ya mitandao (Cyber
Law) iliyoanza kutumika.
"Endapo
kama TCRA watashindwa kumnasa mhusika wa uongo huu wa kuogofya, inabidi
mamlaka husika iangalie upya ajira ya watendaji wake maana kama taasisi
nyeti kama JWTZ inaguswa na wao wakae kimya tu basi ujue kuna tatizo
ambalo inapaswa Serikali ilifanyie kazi", amesema msomaji mmoja wa Globu
ya Jamii katika maoni yake.
0 comments:
Post a Comment