Ivan
Matovu akisherehesha harambee ya Childbirth Survival International
iliyofanywa kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani siku
ya Jumamosi Septemba 12, 2015 katika chumba cha mkutano cha Nyerere
ndani ya jengo la Ubalozi huo na jumla ya $2,696 zilikusanywa siku hiyo
kwa ajili ya kusaidia kuokoa maisha ya wazazi wanaotarajia kujifungua
katika Hospitali ya Wilaya ya Biharamuro. CSI walishawahi toa msaada wa
namna hiyo hospitali ya Amana iliyopo Wilaya ya Ilala jijini Dar na
nchini Uganda kwa lengo hilo la kuokoa maisha ya wazazi watarajiwa wa
kujifungua. Takribani ya wazazi 35 hufa kila siku aidha kwa sababu ya
kukosekana vifaa au kwa uzembe na kutokuwepo kwa elimu ya kutosha
itakayosaidia kuokoa maisha ya mzazi hao. Na kama ingekua daladala kila
siku inatokea ajali na kuua wa 35 nadhani nchi ingacha shughuli zake na
kulitazama swala hilo kwa upana zaidi lakini mtizamo wa akina mama hao
35 wanaopoteza maisha kila siku kwa ajili ya kujifungua bado wananchi na
serikali haijalichukulia swala hili uzito unaostahili ya kuokoa maisha
ya akina mama hao. PICHA NA VIJIMAMBO NA KWANZA PRODUCTION
Tausi
Swedi mmoja ya waanzilishi wa CSI akielezea kazi kubwa inayofanywa na
Childbirth Survival International kujaribu kuokoa maisha ya akina mama
wanaojifungua.
Mkurugenzi
na mmoja ya waanzilishi wa CSI nchini Tanzania Mama Stella Mpanda
akielezea kazi ya Childbith Survival International nchini Tanzania.
Sandra Kiyonga mmoja wa CSI akielezea jambo.
Jessica
Mushala akiipongeza CSI kwa kazi kubwa na nzuri ya kuwasaidia akina
mama wanaojifungua Duniani kote kwa kutoa elimu ya uzazi na vifaa kwa
wazazi na wakunga kujaribu kuokoa maisha ya wazazi wanaojifungua
kutokana na uzembe au kutokua na vifaa ikiwemo elimu ya uzazi.
Kikundi cha utamaduni cha ngoma ya asili aina ya mbuutu ya Uganda ikitumbuiza kwenye harambee hiyo.
Wahudhuriaji kwenye harambee hiyo. Kwa picha zaidi bofya HAPA
0 comments:
Post a Comment