Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Friday, August 5, 2016

MAMA SHUJAA WA CHAKULA ATEMBELEA ULAYA

 Mama Shujaa wa Chakula, Carolina Chelele (Kulia), Mkurugenzi wa Oxfam International Winnie Byanyima wakifanya mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari baada ya kushiriki katika jukwaa la ‘European Development Days' - Brussels, Ubelgiji.
 Picha ya pamoja na Mama Shujaa wa Chakula akiwa The Hague Uholanzi mwezi Juni mwaka huu ambapo alikutana na viongozi, watunga sera na wadau mbalimbali na kuzungumza nao kuhusu uwekezaji kwa wakulima wadogo wanawake
Mama Shujaa wa Chakula Carolina Chelele akishiriki katika jukwaa la ‘European Development Days’ - Brussels, Ubelgiji.

Aliyekuwa mshindi wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu wa nne, Carolina Chelele alipata fursa ya kutembelea nchi za Uholanzi na Ubelgiji mwezi Juni mwaka huu ambapo alifanikiwa kukutana na viongozi, watunga sera na wadau mbalimbali na kuzungumza nao kuhusu uwekezaji kwa wakulima wadogo wanawake.
Akiwa The Hague nchini Uholanzi aliongea na Wataalam wa maswala ya usalama wa chakula na jinsia kutoka wizara ya mambo ya nje na akakutana pia na wawakilishi wa Bunge kutoka kitengo cha maendeleo ya kimataifa cha Uholanzi.
Akiwa Brussels, Ubelgiji Carolina alishiriki katika jukwaa la ‘European Development Days’ ambapo yeye na mkurugenzi wa shirika la Oxfam Winnie Byanyima walishiriki kwenye paneli pamoja na kisha kufanya mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari.
Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaratibiwa na shirika la Oxfam na hufanyika katika nchi za Tanzania, Ethiopia na Nigeria likiwa na lengo la kutambua mchango wa wakulima wadogo wanawake. Kwa Tanzania, shindano hili limeingia msimu wa tano mwaka huu ambapo mshindi atajishindia vifaa vya kilimo vyenye thamani ya shilingi milioni 25.

Like Page Bofya hapa 
www.facebook.com/oxfamtanzania

Twitter
www.twitter.com/oxfamtz

0 comments: