BALOZI FATMA AWASILISHA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO NCHINI QATAR
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mhe.
Fatma Mohammed Rajab, Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
nchini Qatar akiwa katika mazungumzo na Mhe. Sultan bin Saad Al
Muraikhi, Waziri wa Nchi, Mambo ya Nje wa Qatar. Mazungumzo hayo
yalifanyika baada ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho. Wawili
hao walizungumza masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania
na Qatar.
Balozi Mteule wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma Mohammed Rajab akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Sultan bin Saad Al Muraikhi, Waziri wa Nchi, Mambo ya Nje wa Qatar ofisini kwa Mhe. Waziri. Mhe. Fatma Rajab anakuwa Balozi Mkazi wa kwanza kuiwakilisha Tanzania katika Taifa la Qatar. Mhe. Balozi alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Doha alipokelewa
na Idara ya Itifaki ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar. Aidha,
wawakilishi wa Watanzania wanaoishi nchini humo walifika Uwanja wa Ndege
kumlaki
Mhe. Balozi Fatma Mohammed Rajab, akiwa na viongozi wa Watanzania wanaishi nchini Qatar.
0 comments:
Post a Comment