Flora Mbasha akiwa na Mume wake Mpenzi muda mchache kabla hawajaanza safari ya kuelekea Marekani kwa ajili ya ziara yao ya kueneza Injili kwa njia ya uimbaji.
Akiwa anawaaga ndugu jamaa na marafiki katika Ukurasa wake wa Facebook aliandika hivi:
"Bwana Yesu asifiwe rafiki zangu, ninapenda kuwaaga, tunasafiri kwenda Nchini Marekani tutakuwa na ziara huko. tunahitaji maombi yenu sana, tutakuwa tukiwajulisha kila kinachoendelea huko. tunawapenda sana. mbarikiwe. Enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri injili kwa kila kiumbe, aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa"
Wakiwa wamefika Marekani na kupokelewa na wenyeji wao
Ilikuwa ni kipindi ambacho John Gibson anaandika nyimbo ambazo Florah Mbasha atatumbuiza usiku huo
Wakifanya mazoezi kabla ya kuingika katika Tamasha huko DC
Wakiwa na Nyuso za Furaha na wenyeji wao baada ya Tamasha lao kufana
Flora Mbasha akiwa anaimba kwa Hisia na upako wakati wa Tamasha hilo lililo fanyika huko DC
Wakiendelea kumsifu Bwana kwa nyimbo za Injili
Flora Mbasha akimkabidhi CD yake mpya Mchungaji Ramsey baada ya ibada kumalizika
Endelea kufuatilia tukio zima la Safari yao huko DC








0 comments:
Post a Comment