Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Saturday, April 28, 2012

UBALOZI WA TANZANIA NAIROBI WAADHIMISHA SIKU YA MUUNGAMO ( UNION DAY)


Balozi wa Tanzania nchini Kenya,Mh. Batilda S. Burian akisoma hotuba fupi wakati wa kuadhimisha siku ya Muungano ( Union Day) tarehe 26 April 2011 katika ukumbi wa Safari Club,jijini  Nairobi. Maadhimisho hayo ambayo yalihudhuriwa na takriban Mabalozi na jumuiya mbalimbali za umoja wa Mataifa, yalipata pia baraka za uwepo wa Mh. Dr. Abdulla J. Saadalla, Naibu Waziri, WiZara ya Afrika Mashariki pamoja na Wabunge wa Tanzania wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya,Mh. Batilda Burhan akimkaribisha Balozi wa Ghana nchini Kenya ambaye pia anaiwakilisha Tanzania kutokea Nairobi,Mh. Kingsley Karimu kwenye hafla hiyo.
Sehemu ya wageni waalikwa wakishiriki katika toast.
Mh. Balozi akiwa katika picha ya Pamoja na TIMU nzima ya Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya mara baada ya kuhitimisha shughuli nzima ya Maadhimisho ya Miaka 48 ya Siku ya Muungano ( Union Day).

0 comments: