Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Friday, May 4, 2012

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA BARRICK GOLD MINE WAMZUIA MWANAHARAKATI KUTOKA TANZANIA KUHUDHURIA


Amani Mustafa Mhinda akiwa na wanaharakati wengine nje ya jengo.
Amani Mustafa Mhinda akiwa anawautubia wanaharakati nje ya jengo ambako mkutano wa barrick ulifanyika.
Wanaharakati na wahandamanaji waliokuwa nje ya jengo ambalo mkutano wa Baarrick ulifanyika.
Baadhi ya wanaharakati wakiwa na mabango yao nje ya jengo ambalo mkutano wa barrick ulifanyika.

--
Mkutano
wa mwaka huu wa Barrick Gold Mine uliofanyika Toronto Nchini Canada May
3, 2012, ulimzuia Mwanaharakati wa Haki za binadamu na mwanasheria wa
masuala ya Maliasili Mr. Amani Mustafa Mhinda, ambaye pia ni Mkurugenzi
wa asasi ya kijamii ya HAKIMADINI,inayoshughulika na haki za binadamu
katika maeneo ya machimbo ya madini.

Mhinda
alikuwa amedhamiria kueleza wahudhuriaji wa Mkutano huo kuhusu umuhimu
wa  kujenga uwezo wa wachimbaji wadogo na jamii zinazoishi katika
maeneo ya machimbo, ili ziweze kunufaika na rasilimali ya madini ya
Tanzania, pamoja na kulinda na kutetea haki zao, ambayo pia ni agenda
kuu ya HAKIMADINI yenye makao yake makuu mjini Arusha. 
  
Pamoja na kuwa na ajenda hiyo,  Barrick Gold na uongozi wake walimzuia kuingia  katika eneo la mkutano huo.
kinukuliwa
na gazeti moja la kitaifa la Canada liitwalo The Canadian, Mhinda
alieleza  uhalali wake wa kuhudhuria mkutano huu huku akinukuu matukio
ya uvunjwaji wa haki za binadamu yanayofanywa na makampuni ya uchimbaji

“Kama
shirika lisilo la kiserikali la kitanzania na wananchi wa Tanzania,
tunataka kuona mauaji   na uvunjwaji wa haki za binadamu  unaohusishwa
na makampuni ya uchimbaji madini ya Canada yanamalizwa. Niko hapa
kumwakilisha watanzania wengi ambao ni wahanga  wa mgodi huu pamoja na
Mama Otaigo, aliyefariki mwezi wa nne kwa kunywa maji yenye sumu
yaliyopo karibu na Mgodi wa North Mara”.

 Amani alisema
Mwanaharakati
huyo pamoja na wanaharakati wengine wa masuala ya haki za binadamu
walinyimwa kuzungumza kuhusu matendo ya kinyanyasaji yanayofanyika
kwenye maeneo ya machimbo ya  madini nchini Tanzania katika mkutano
 Mkuu wa Mwaka wa Barrick Gold mine.

Hatua
hiyo ya kampuni ya Barrick Gold Mine kuwazuia wanaharakati wa Tanzania
na  kuwaruhusu wenzao wa nchi kama Papua New Guines na Chile
kuliushangaza umati wa waalikwa kwenye mkutano huo.

Mhinda
alishutumu hatua iliyochukuliwa na Barick Gold ya kumzuia kuingia
katika mkutano huo kama “juhudi za wazi za kuficha uvunjwaji wa haki za
binadamu unaofanywa na makampuni ya uchimbaji na wawekezaji wengine kwa
jamii za kitanzania".

Pamoja
na kufungiwa kuingia katika mkutano huo, Amani na wanaharakati wengine
walipata nafasi ya kuelezea habari zao kwa maelfu ya watu
waliokusanyika nje ya eneo la Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Barrick kwa
ajili ya kupinga unyanyasaji unaofanywa na kampuni ya Barrick Gold
ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya uchimbaji dhahabu duniani,
iliyoanzishwa na kusimamiwa na Peter Munk. 

Miongoni
mwa wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo ni pamoja na Waziri mkuu wa zamani
wa Canada. Barick hupata fedha za serikali na misaada ya kidiplomasia.
Makao makuu ya barrack yapo Toronto, Canada, wakati  Africa Barrick, ni
kampuni ya Uingereza ambayo humilikiwa kwa 70% na Barrick Gold

0 comments: