Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Monday, December 10, 2012

Msiba wa Baba Mzazi wa mwanajumuiya Grace Mwasokwa. Harlem , New York





Wanajumuiya,
Tunasikitika kutangaza kifo cha Mzee Joseph Mwasokwa (72), Baba mzazi wa dada yetu Grace Mwasokwa amefariki Jumamosi Desemba 9th, 2012  usiku nje ya geti la nyumbani kwake,mjini Mbeya. 


Marehemu atazikwa Jumanne Desemba 11, 2012 kijijini kwake Kyela. Ameacha Mjane, watoto  7 na wajukuu. Alikuwa mpenzi sana wa soka na timu ya Yanga. Mwenyezi Mungu aipokee roho ya Marehemu na ailaze mahala pema -Amin.

Kama ilivyo ada, tunaombwa sote kwa umoja wetu na upendo tufike kwa Dada Grace kumpa pole na kutoa ushirikiano wetu wa kiroho na wa dhati katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo ya Baba yetu mpendwa!

Address: 2855 8th Avenue apt. 2C
             New York, NY 10039 (Harlem)
             btn 152nd & 153rd Street on 8th Avenue (Frederick Douglas Avenue)- Harlem
             Tel. (347)422-3297 au (347)712-8539
"Bwana ametoa na  Bwana ametwaa jina lake  lihimidiwe. Amina”
Raha ya Milele Umpe Eee Bwana na Mwanga wa Milele Umuangazie apumzike kwa amani. Amina

0 comments: