Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Monday, August 12, 2013

SHEREHE ZA MIAKA 5 YA KANISA LA THE WAY OF THE CROSS GOSPEL MINISTRIES ZAFANA


Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata  Mulamula ndiye aliyekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 5 ya kanisa la The Way of The Cross Gospel Ministries yaliyofanyika kwenye kanisa hilo College Park Maryland na kuhudhuriwa na watu mbalimbali kutoka DMV na majimbo ya jirani. Maadhimisho haya yalianzia Ijumaa na Jana Jumapili Aug 11, 2013 ndiyo ilikua hitimisho lililoambatama sala, nyimbo za injili kutoka vikundi mbalimbali wakiwemo waimbaji wa nyimbo za injili toka Tanzania Upendo Kilahiro na Christina Shusho waliokuja maalum kwenye maadhimisho hayo.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa utawalawa na fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula na Dr Nicku Kyangu Mordi.
Meza kuu katika picha ya pamoja kwenye maadhimisho ya miaka 5 ya kanisa la The Way of The cross Gospel Ministries yaliyofikia mwisho siku ya Jumapili Aug 11, 2013 College Park Maryland.
Juu na chini ni Mhe. Balozi Mulamula akiongea na Watanzania waliohudhuria maadhimisho hayo ya miaka 5 ya kanisa la The Way of The Cross Gospel Ministries yaliyofikia mwisho siku ya Jumapili Aug 11, 2013 College Park, Maryland.
Wachungaji kutoka makanisa mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo ya miaka 5 katika picha ya pamoja.
Upendo Kilahiro, mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Tanzania akipamba jukwaa kwa nyimbo mbalimbali siku ya mwisho  maadhimisho hayo siku ya  Jumapili Aug 11, 2013, College Park, Maryland.
Mwimbaji wa nyimbo za injili toka Tanzania, Christina Shusho akiimba moja ya nyimbo zake siku ya mwisho ya maadhimisho ya miaka 5 ya kanisa la The Way of The Cross Gospel Ministries yaliyofanyika Jumapili Aug 11, 2013, College Park Maryland.

0 comments: