Dr. Slaa akiwa na mchumba wake Bi. Josephine Mshumbuzi katika picha ya pamoja na na viongozi wa Chuo cha Tiba
Dr. Slaa na Dean wakiwa kwenye maongezi ya kufanya kazi pamoja
Dr. Slaa akipewa maelekezo na rais wa chuo cha Tiba kulia ni mchumba wwake Bi. Josephine Mshumbuzi.
Dr. Slaa akielekezwa kwenye chumba cha Mikutano na rais wa chuo cha
tiba huku wakiwa wamefuatana na mchumba wake Bi. Josephine Mshumbuzi.
Dr. Slaa akiongozwa na Professor ambaye pia ni dean msaidizi pamoja na mchumba wake Josephine Mshumbuzi.
Akiwa
anaendelea na ziara yake nchini Marekani, siku ya ijumaa katibu mkuu wa
chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dr. Wilibrod Slaa alitembelea
Chuo kikuu cha tiba cha Alabama ambako alilakiwa na viongozi wa juu wa
chuo hicho
Chuo
kikuu cha Alabama ina wanafunzi 16,000 katika Kitengo cha tiba. Hii
ndio moja ya vyuo vikubwa nchini marekani katika maswala ya tiba, ikiwa
na vitengo karibia vyote vinavyotibu magonjwa mbali mbali. Chuo hicho
pia ufanya utafiti nchi nyingi duniani husasan afrika. Chuo hicho
ushirikiana na nchi kama Afrika kusini, Zambia, Malawi, na Aljeria
katika mambo ya utafiti na kutayarisha watafiti. Kadhalika imekuwa
ikisaidia mataifa kama Saudi Arabia, Uchina na Qatar kutayarisha
madaktari bingwa
Ikiwa
ni moja ya sera za chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kuweka
mikakati ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya huduma bora za afya kwa
watanzania, Dr. Slaa Amekuwa akizunguka nchini marekani ili kujifunza
mambo mbali mbali hasa mafanikio ya vyuo kama hivi, na ni jinsi gani
anaweza kupata ushirikiano na vyuo hivi ili kutayarisha madaktari wengi
wa tiba na mabingwa ili kuiokoa taifa gharama kubwa ya kuwapeleka
wagonjwa nje ya nchi.
Kujibu
ombi la Dr. Slaa, rais wa chuo cha tiba, ameahidi kushirikiana na
serikali ya Tanzania chini ya CHADEMA ili kujenga vyuo vya utafiti na
tiba nchini Tanzania. Viongozi hao wameweka bayana nia yao ya kuisaidia
Tanzania hasa ufisadi na urasimu uliopo utaondolewa. Naye kwa upande
wake, Dr. Slaa amemuahidi kwamba, ufisadi utakuwa ni historia katika
serikali ya CHADEMA.
Chuo
hicho itakuwa tayari kuwatuma madaktari wake bingwa wa kila aina nchini
Tanzania kusaidia katika mambo mbali mbali ya tiba itakayoambata na
makubaliano na serikali ya CHADEMA ikiwemo kuwafundisha na kuwatayarisha
madaktari 4,000 katika kipindi cha miaka (accelerated program) miwili
kama walivyofanya nchini Bangladesh ili kupunguza uhaba wa madaktari.
Hawa ni madaktari wasaidizi ambao wanaujuza Fulani. Madaktari wengine
watahitaji miaka mitatu ili kuwa madaktari bingwa.
0 comments:
Post a Comment