NAIBU KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI MH. MWIGULU NCHEMBA (MB) AUNGURUMA NCHINI UINGEREZA NA KUONYESHA UKOMAVU WAKE KIFIKRA.
- “Mabadiliko hayatakuja kwa kubadilisha vyama bali ni nia zenu {Mindset) zikifanywa kuwa mpya na mapenzi ya nchi yenu.”
Katika hali iliyotajwa kuwa ni ya furaha, kutokana na changamoto
zilizokuwepo siku ya jumamosi jijini Leicester Uingereza, kijana shupavu
na “JEMBE” la kujivunia katika Taifa la Tanzania Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Taifa, na Mbunge wa Ilamba Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Lameck
Nchemba akiambatana na mshauri wa Rais mheshimiwa Rajabu Luhwavi, kwa
pamoja waliweza kutoa majibu ya changamoto nyingi zinazolikabili Taifa
kwa watanzania wengi waliojitokeza katika mkutano mkubwa uliohudhuriwa
na watanzania wengi kutoka maeneo mbali mbali ya Uingereza.
Ujasiri, uwazi na ukweli wa mambo ya kiutendaji katika taifa letu ndio hasa imekuwa ni chachu na kivutio kikubwa kwa
watanzania
wengi waliohudhuria mkutano huo mkubwa jiji Leicester ambapo Mh.
Mwigulu Nchemba aliweza kuweka wazi mengi ambayo serikali imeweza
kuyafanya katika upande wa Elimu, Miundo mbinu na huduma za afya kwa
watanzania pia kutoa kasoro katika maeneo yanayokuwa vikwazo katika
kutoa huduma bora.
“Nchi yetu ipo katika mchakato wa kupata katiba mpya, mojawapo ya
mambo ambayo tunayafanyia kazi ni suala la uraia pacha. Ni pendekezo
lililowakirishwa na Chama Cha Mapinduzi katika baraza zake za uchangiaji
maoni ya Katiba mpya. CCM inawajali watanzania wote hivyo ikaona ni
vyema na nyinyi mlioko ughaibuni kupata fursa sawa za kimaendeleo katika
nchi yenu” alisema Mhe. Mwigulu Nchemba.
Mheshimiwa Nchemba aliendelea na kusema kwamba nchi yetu inapita
katika kipindi cha mabadiliko. Idadi ya watanzania imeongezeka kwa kiasi
kikubwa na wengi wa ongezeko hili ni vijana ambao ni watafutaji na
wajasiliamali wengi. Kuna haja kubwa kama chama kubuni taratibu nzuri za
kimaendeleo ili kuendana na wimbi hili la ongezeko la watu.
Mheshimiwa Nchemba kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi aliwasihi
watanzania waishio Uingereza kutumia upeo (Exposure) waliyonayo katika
kulisaidia taifa kupiga hatua zaidi za kimaendeleo kuliko kuwa na
ushabiki wa siasa kama ilivyo kwa baadhi ya wanasiasa nyumbani na badala
yake wawe chemichemi ya mawazo ya kimaendeleo katika nchi yao.
Watanzania mlioko nje mna nafasi kubwa ya kuchangia mawazo ya
kujenga taifa lenu la Tanzania, nitawakilisha hoja yenu ya kupatiwa njia
ya kuwakilisha mawazo yenu ama jambo lolote lenye busara na utendaji wa
mabadiliko katika nchi yetu ya Tanzania ili pia mpate fursa ya
kuwakilisha maoni na hoja za haja za kuleta mabadiliko. Kutokuwa na
jukwaa lenu la kuwakilisha hoja zenu za kamandeleo ni kosa. Wazo lolote
la kujenga lazima liwakirishwe katika vikao rasmi kama mchango wa CCM
diaspora, liongeza Mheshimiwa Nchemba.
Tengenezeni ajenda kulingana na ukomavu na upana wenu wa kimawazo
ambao mnaupata katika nchi hizi za Magharibi ambazo zimepiga hatua kubwa
za kimaendeleo kutokana na desturi zao za kuthamini, kujituma na
kutenda kazi zao kwa uadilifu mkubwa kwa mapenzi na nchi zao ili
kuchangia utekelezaji wa sera ya chama katika nchi yetu kwenye sekta
mbalimbali za afya, elimu, miundombinu , sheria n.k. na mimi naahidi
tutatengeneza na kuboresha uwanja mzuri wa mawasiliano kati yetu
aliongeza Mheshimiwa Mwigulu Nchemba.
Mheshimiwa Nchemba pia alisisitiza upendo na umoja baina ya
watanzania na kuwaomba wawe kitu kimoja na akawataka wana CCM Uingereza
kuwa chachu ya kuwaunganisha watanzania wote bila kujali itikadi za
kisiasa na vyama vyao. Mheshimiwa Nchemba pia amekuwa akikonga nyoyo za
watanzania wengi kulingana na utashi na ufahamu wa kujibu maswali
kiufasaha, wazi na kwa uhakika pale alipoulizwa katika mikutano yake
iliyofanyika katika majiji ya Leicester, Northampton na London nchini
Uingereza.
Katika mkutano uliofanyika jijini Leicester watanzania wengi
waliuliza maswali yanayohusu Katiba , Utawala wa Sheria wenye haki sawa
kwa wote kama ilivyo katika nchi za kimagharibi, Uraia pacha, Kurugenzi
inayoshughulikia masuala ya Diasprora ambayo badala ya kuwa kiunganishi
imekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wanadiaspora kutokana huduma mbovu zenye
kutokujali na majivuno kutoka kwa watendaji wake wakuu, Tunashauri
watendaji katika kitengo hiki watokane na wanadiaspora wenyewe kwani
upeo (exposure) wao kiutendaji utaleta ufanisi kuliko ilivyo sasa hivyo
kuleta mchango wao kwa maendeleo ya Taifa. Pia Watanzania hao na wana
CCM wameishauri serikali kubadirisha taratibu zake za kiajira katika
Balozi zetu za nje kwa kuwatumia watanzani wenyeji wa maeneo hayo ili
kupunguza mzigo wa gharama serikali, kuongeza ufanisi kwani uelewa wa
kufanya kazi katika mazingira wanayoishi wanaufahamu vyema zaidi kuliko
kuleta watendaji wote katika Balozi zetu kutoka nyumbani.
Vilevile katika mkutano uliofanyika jijini Northampton siku ya
Jumapili, mengi ya maswali yaliyoulizwa na watanzania waishio katika
jiji hilo ni kama katika masuala ya usalama wa nchi na raia wake dhidi
ya matukio ya tindikali na majanga ya mabomu kule Arusha, tukio la
kigaidi hivi karibuni nchini Kenya na utayari wa nchi yetu katika
kukabiliana na wimbi kama hilo endapo litatokea nchini kwetu, mikakati
ya kupambana na madawa ya kulevya pamoja na lile gonjwa sugu la rushwa.
Akijibu kwa ufasaha maswali hayo Mheshimiwa Rajab Luhwavi ambaye
anaambatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa Mheshimiwa Mwigulu
Nchemba, katika ziara hii, alianza kwa kuwahakikishia usalama wa taifa
Watanzania waliofika katika mkutano huo na kuwaondoa hofu hiyo. Na
kuwajulisha kwamba serikali imeweka mikakati madhubuti ya kupambana na
uhalifu wa aina hiyo na kwamba taratibu za lazima zinafanyika na hali ni
shwari.
Imetolewa na:
Abraham Sangiwa – Deputy Secretary Ideology and Publicity
Chama Cha Mapinduzi Uingereza (CCM UNITED KINGDOM)
Tarehe 08.10.2013.
Katibu
wa Chama cha Mapinduzi tawi la Uingereza Bi. Mariam Mungula akiwa
pamoja na uongozi wa tawi la CCM UK wakimpa “tour” ya London Underground
train (Tubes) Naibu katibu Mkuu CCM TAIFA Mh. Mwigulu Nchemba (MB)
katika ziara yake hapa Uingereza
0 comments:
Post a Comment