Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Monday, May 5, 2014

TAARIFA YA MSIBA PHILADELPHIA, NEW YORK NA TANZANIA

Mama Harriette Peace Kagaruki amefariki dunia huko Philadelphia tarehe 28 Apil 2014. Marehemu alikuwa anaishi Tanzania na alikuwa amekuja Marekani kuwasalimia wanawe Erick Kagaruki (Ohio) na Mary Kagaruki (Philadelphia), na ndipo alipougua ghafla na baadae kuaga dunia.
Marehemu Mama Kagaruki hakuwa mkazi wa Marekani. Kwa maana hiyo na kwa sababu msiba huu umetokea ghafla na kwa sababu ni Mtanzania mwenzetu tunaomba tusaidiane ili tuweze kufanikisha shughuli za msiba huu ili aweze kupelekwa Tanzania. Kwa vile Marehemu alikuja kutoka Tanzania kutembelea wanawe hana rafiki au watu wa kumsaidia kufanikisha msiba wake hivyo msiba huu ni wetu Watanzania wote waishio Marekani, wewe na mimi. Hivyo tunawaomba muonyeshe ukarimu wenu ili msiba huu uweze kufanikiwa. Kiasi cha dolla 20,000 kinahitajika na tunawaomba mtoe michango ili tuweze kufikisha kiasi hicho. Toeni Kupitia Account Number ifuatayo:
Wells Fargo Bank
Routing #: 031000503
Account# 6595913119

Jina la mwenye akaunti ni la Mtoto wa Marehemu: Mary Kagaruki

Marehemu kwa sasa yuko:
Funeral Home
366 West Lancaster Avenue
Wayne PA 19087

Kwa taarifa zaidi za msiba huu wasiliana na:
Erick Kagaruki – 937-361-4189
Mary Kagaruki – 267-963-8190
Abbas Babyusha – 914-584-7502
Doris Rweyemamu – 646-379-9135
Kwa wale wasioweza kutoka michango kwenye akaunti iliyotajwa hapo juu mnaweza kufika ubalozi New York na kumkabidhi Ms. Doris Rweyemamu michango yenu na simu yake ni 646-379-9135. Doris atakusanya vile vile michango ya Watu   wa Mount Vernon akisaidiwa na Abbas Byabusha (914-584-7502).
Dr. Temba  (347-489-6532) na Raphael Faida (347-869-2230) nao watakuwa wakikusanya michango kutoka kwa Wanajumuiya.
Tunawaomba Watanzania wote wa Marekani watusaidie kwa kutoa michango ili tufanikishe shughuli za msiba huu.
Kwa niaba ya Familia ya Wafiwa na Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania,
Deogratius Mhella,
Katibu, New York Tanzanian Community.

0 comments: