Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Monday, June 9, 2014

HARAMBEE YA KUMCHANGIA NDUGU ERICK BAHUNDE YAFANA DMV, NI YULE NDUGU ALIYEPATA AJALI NA KUKATIKA MIGUU YOTE MIWILI PAMOJA NA MKONO WA KUSHOTO.



Bwna Erick Elisha Bahunde picha akiwa  hospitali wakati alipopatwa na ajali Photo Via Vijimambo
Na Abou Sharty Washington DC
Jumuiya ya waTanzani waishio DMV imeweza kushirikiana katika harambe ya kumchangia ndugu yetu, Erick Elisha Bahunde ambaye alipatwa na ajali mbaya wakati alipokuwa akiwajibika kazini na kukatika miguu yake yote miwili pamoja na mkono wa kushoto, mnamo February 2014. katika  Jimbo la Indiana nchini Marekani.

Harambe hiyo ulioyongozwa na wana jumuiya wa hapa DMV akiwemu MC Saidi Mwamende, Katibu wa Jumuiya ya waTanzania , Amos Cherehani, Mchungaji Malekela Ndugu Faraja Isingo, Mashaka Bilali pamoja na Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV Bwna Iddi Sandaly.
Watanzania mbali mbali walihudhuria katika harambe hiyo iliofunguliwa rasmi kwa dua iliyoombwa na Mchungaji Malekela, na pia kuwaasa watanzania kushirikiana kwa hali na mali pale mtu yoyote atakaefikwa na  misukosuko yoyote ile ambayo anastahili kusaidiwa asaidiwe. 

Mchungaji Malekela aliendelea kwa kusema kuwa ''Mungu amesema kwamba kama mwanaadamu anatafuta kuwa na dini safi basi dini safi ndio hii''  kwa kuweza kujitolea kuwahudumia Wajane, Masikini, Mayatima na wahitaji wasiyojiweza kama wagonjwa n.k, huku akikumbusha kwamba ''Mungu ataendelea kugusa watu'' na pia kuwataka waliohudhuria katika ukumbu huo  kuchochea gharama dhidi ya kumchangia mtarajiwa anaestahiki kuchangiwa.

Baada ya ufunguzi kwa maneno ya Mungu, waTanzani waliohudhuria katika harambee hiyo walianza kuchangia michango mbalimbali zikiwemo pesa taslim, cheki pamoja na vitu ama bidha mbalimbali vilizofikishwa ndani ya ukumbi huo, pia wale walioahidi kutoa michango na kuandika idadi ya kiwango cha pesa watakazozitoa walijumuika pamoja na kuaza kutoa michango hiyo, huku katibu wa jumuiya ya waTanzania DMV  Bwna Amos Cherehani  pamoja na Mashaka Bilal wakisherehesha shuhuli hiyo kwa  uuzaji wa kunadi bidhaa hizo zilizofikishwa katika harambee hiyo.

Kulikuwa na uzwaji wa bidhaa tofauti zilizoletwa na wana waTanzania waishio hapa DMV zikiwemo vitenge, kanga, gauni, saa za ukutani kopo za kahawa ya kinyumbani, vitu vyote hivyo viliuzwa na hakuna hata kimoja kilichobakia katika harambe hiyo na kutimiza kiwango cha $ 4.800 dhidi ya watu wachache waliohudhuria katika Harambee hiyo ilioandalidwa na Familia ya Erick Elisha pamoja na Jumuiya ya waTanzania DMV, Siku ya Jumapili June 8, ndani ya ukumbi wa Sligo Creek uliopo Silver Spring Maryland Nchini Marekani.

Aidhi Bwna Erick Elisha Bahunde  aliwashukuru wale wote waliotoa michango yao kwa hali na mali kwa kuweza kukamilisha harambee hiyo kwa upendo wao mkubwa na kujisikia furaha kwa michango hiyo aliyoipa kwa watanzania wenzake wanaoishi hapa Washington DC.

VIDEO NA PICHA : MUACHE MUNGU AITWE MUNGU NA KAMA HUJAFA HUJAUMBIKA‏  
Mtanzania Elisha Bahunde jina maarufu Eric ambaye siku ya Jumamosi Feb 15, 2014 alipata ajali Jimbo la Indiana iliyopelekea kukatika kwa miguu yote miwili na mkono wa kulia na baadae kuhamishiwa Jimbo la Maryland kwa matibabu zaidi kwa sasa yupo University Of Maryland Medical Center iliyopo 22 S Greene St, Baltimore, MD Ghorofa ya 6 chumba # 8 na anatumia jina la Elisha Bahunde ama kweli hujafa hujaumbika na Mwenyezi Mungu ndiye mueza wa kila jambo ebu sikiliza mwenyewe video hiyo hapo chini na ujionee na picha pia tumekuekea video aliyoshiriki kwenye Kijiwe cha Ughaibuni ameva shati la njano na amekaa karibu na Ally Bambino


 Elisha Bahunde akiwa chumba # 8 ghorofa ya 6 alipolazwa tangia siku ya Jumatano Feb 19, 2014 alipoletwa Maryland kwa matibabu zaidi
 Elisha Bahunde au Eric akiwa hana miguu wa mkono kama picha inavyoonyesha.
 Rais wa Jumuiya DMV, Bwn. Idd Sandaly akiwa Hospitalini hapo kumjulia hali mgojwa
 Abdi Makeo amkimjulia hali Elisha Bahunde
 Said Mwamende akimjulia hali Bwn. Eric huku akilengwa na machozi
 Wanajumuiya waliofika kumjulia hali wakiwa hawaamini walichokiona.
Kutoka kushoto ni Abdi Makeo, Saidi Mwamende, Rais wa DMV Idd Sandaly na Jabir Jongo wakiwa chamba cha mapumziko baada ya kumaliza kumjulia hali Elisha Bahunde kwa jina lingine Eric
Kijiwe No. 44 from Luke Joe on Vimeo.

0 comments: