Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Tuesday, June 10, 2014

SOMA MAJINA YA WAGOMBEA UONGOZI JUMUIYA YA WATANZANIA DMV


KAMATI MAALUM YA UCHAGUZI- DMV

TANGAZO RASMI:
MAJINA YA WAGOMBEA UONGOZI KATIKA JUMUIYA YA WATANZANIA DMV 2014.

RAIS:                                                                  MAKAMU WA RAIS:
1.     IDDY SANDALY                                       1. HARIETT SHANGARAI
2.     LIBERATUS MWANG’OMBE               2. SALIMA SULEIMAN

KATIBU:                                                            MAKAMU WA KATIBU:
1.     SAID MWAMENDE                                1. SOLOMON CRIS
2.     ISMAIL MWILIMA

MWEKA HAZINA                                             MAKAMU WA MWEKA HAZINA
1.     JASMINE RUBAMA                               1. JACOB KINYEMI



Kamati ya Uchaguzi wa viongozi wa Jumuia ya Watanzania- Washington Metro (ATC), inawatangazia kuwa uchaguzi ufanyika JULY 20, 2014 kuanzia saa saba mchana hadi saa kumi na mbili, anuani ya ukumbi utatangazwa baadaye.
Taratibu zitakuwa kama zifuatazo:

1.     JUNE 19, 2014 ni tarehe ya mwisho kupokea malipo ya ada kwa wale watakaoshiriki kupiga kura; kwa mujibu wa katiba kila mpiga kura au mgombea wa uongozi wa Jumuiya lazima wawe wanachama hai kwa siku zisizopungua thelathini.
2.     Hakuna malipo yeyote yatakayopokewa mlangoni siku hiyo ya kupiga kura.
3.     Ukitaka kulipia ada yako tembelele tovuti ya jumuiya utapata maelezo au tutumie barua pepe uchaguzi2014@gmail.com na tutakusadia kulipia ada yako na kuwa na haki ya kupiga kura.
4.     Kama ulilipia kwa mwezi mmoja kumbuka kulipia mara ifikapo tarehe hiyo mwezi unaofuata,mfano kama ulijiunga au kuongeza muda wako June 6, 2014 uanachama wako unakoma siku July 6, 2014, ili uweze kupiga kura July 20, 2014 itakubidi ufanye malipo mengine ya ada ($10) kabla ya July 6, 2014.
5.     Kamati inawatangaza rasmi wagombea hapo juu na wagombea wanaweza kuanza kampeni kuanzia June 10, 2014.

Tunashukuru kwa ushirikiano wenu,

Kamati maalum ya Uchaguzi DMV 2014.

0 comments: