Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula
akitambulisha Mhe. Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo kwa
Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama
Lily Munanka siku ya Jumatatu June 9, 2014 Waziri wa Nishati na Madini
na ujumbe wake walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ulipo
mtaa wa 22, jijini Washington, DC.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula
akitambulisha Mhe. Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo kwa
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Idd Sandaly siku ya Jumatatu
June 9, 2014 Waziri wa Nishati na Madini na ujumbe wake walipotembelea
Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ulipo mtaa wa 22, jijini Washington,
DC.
Mkuu wa Utawala na Fedha, Mama Lily Munanka akiongea machache huku
akimshukuru Mhe. Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo na
Ujumbe wake kukubali kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na
baadae kumkaribisha Balozi Liberata Mulamula kuongea maneno machache.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula akiongea
machache na kumshukuru Mhe. Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter
Muhongo na Ujumbe wake kwa kukubali kutembelea Ubalozi wa Tanzania
nchini Marekani na baadae kumkaribisha Mhe. Waziri kuongea machache na
Maafisa, na Wafanyakazi wa Ubalozi huo wakiwemo wanajumuiya.
Mhe. Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo akiongea
machache na kumshukuru Mhe. Balozi Liberata Mulamula kwa makaribisho
mazuri na kuelezea sababu ya ujio wake nchini Marekani ambao alianzia
New York kwenye mkutano wa mwongo wa Nishati Endelevu kwa wote (SE4ALL) ambao Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, siku ya alhamisi wiki iliyopita aliuzindua
rasmi mkutano uliohudhuriwa na wajumbe zaidi wa 1,000 wakiwamo
zaidi ya mawaziri 20 wa Nishati, wafanyabishara, mashirika ya kimataifa
yakiwamo ya fedha na Asasi zisizokuwa za kiserikali,
Ujumbe
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huu ambao ulianza
Juni 4 na kumalizikaJuni 6, uliongozwa na Waziri wa Nishani na Madini
Professor Sospeter Muhongo ambaye pamoja na kuhudhuria na kuchangia
mijadala mbalimbali, ijumaa ( June 6), alizungumza katika mkutano
wa mawaziri kuhusu nafasi ya Nishati katika Ajenda za Maendeleo
Endelevu baada ya 2015 na utayari
wa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa Bara la Afrika kuhushu Nishati
Endelevu kwa wote unaotarajiwa kufanyika mapema mwakani.
Picha ya pamoja ya Waheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na mwenyeji wake Balozi Liberata Mulamula.
Waheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na
mwenyeji wake Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Maafisa
na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Waheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na
mwenyeji wake Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Ujumbe
aliokuja nao Mhe. Waziri wa Nishati na Madini kutoka kushoto ni
Eng.Jones Olotu(Rural Energy Agency wa Wizara ya Nishati na Madini),
Eng. Rwatabangi P. Luteganya (Manager Investment TANESCO), Styden
Rwebangila (Energy Engineer Wizara ya Nishati na Madini), Venosa Ngowi
(Senior Petroleum Geologist TPDC), Eng. Leonard R. Masanja (Director
TANESCO Board of Directors) na Eng. Yahaya I. Samamba (private Secretary
to Minister Wizara ya Nishati na Madini)
Waheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na
mwenyeji wake Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na
Wanajumuiya DMV. Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Waheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na mwenyeji wake Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CCM tawi la DMV
Waheshimiwa Waziri wa Nishati na
Madini Prof. Sospeter Muhongo mwenyeji wake Balozi Liberata Mulamula
wakijipatia chakula cha jioni ambacho kiliandaliwa na Edah Gachuma.
Picha zote na Vijimambo Blog
0 comments:
Post a Comment