
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu waTanzania Mhe Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake walipomtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.
Jaji
Mkuu na ujumbe wake wako Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na
mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa
kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington na pia
kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika
ili kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. Wengine kutoka
kushoto ni Balozi wa Tanzania
nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula, Jaji wa Mahakama ya rufani Mhe
Ibrahim Juma, Msajili wa Mahakama Kuu Mhe Ignass Kitusi,daktari wa Rais
Profesa Mohamed Janabi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mhe Hussein Katanga.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Kushoto ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

Rais Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman.Picha na Ikulu
0 comments:
Post a Comment