Msichana
wa kitanzania, Rose Mmbaga ameweza kushinda tuzo ya Mwanamke mwenye
Ushawishi ‘Women in Events Hall of Fame’ ya nchini Marekani na kuwa ni
Mwafrika pekee katika kusaidia vijana katika maswala ya masuala ya
Mazingira.
Mmbaga ameshinda tuzo hiyo kutokana na uwezo wake wa ushawishi katika kazi za kijamii ambazo amezifanya nchi nzima.
Amesema
kuwa Safari yake ilianza na kujitolea kwa takribani miaka mitatu
baada ya kuona ajira zinasumbua, na alianza na VSO international kwenye
mradi wa International Citizen Service alafu nikajiunga na Restless
development katika mradi wa kijana tung’are kazini chini ya
International Citizen Service programu kwa takribani miezi sita na tena
nikaenda Raleigh Tanzania kwenye mradi wa Expedition.
“nilijenga
shule kusaidia watoto yatima,mashirika yote nilishirikiana na vijana
kutoka ndani na nje ya nchi na miradi ilifadhiliwa na DFID yani serikali
ya wingereza.Haikua rahisi lakini leo hii naweza kuona matunda ya
kujitolea katika jamii yangu.”amesema Rose.
Kupitia
safari yangu leo hii nimeweza kupata tuzo ya kimataifa kutoka
Association for women in events,Hall of fame kama “Woman of
Influence”(Mwanamke mwenye ushawishi) ambayo walioniwezesha ni watu
ambao wanafahamu kazi yangu na nilioshirikiana nao katika kazi zangu
haswa vijana wa kitanzania na wengi wao ni wale waliojitolea
Amesema
pongezi zinamwendea mwanaharakati wa kuwasaidia wanawake duniani Mandy
Sanghera ameweza kuwa wa kwanza kuninominate jina langu kati ya wanawake
wengi na leo hii ninamshukuru kwa kupitia yeye nimeweza kushinda.
0 comments:
Post a Comment