Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Saturday, May 19, 2012

WATANZANIA MJINI ROMA ITALIA WAUAGA MWILI WA MAREHEMU FR. JAMES A. MBWANA

Mwili wa Marehemu James Mbwana Ukitolewa kanisani na mapadri wakitanzania.
Watanzania kutoka kila kona ya Roma nchini Italia, wakiongozwa na balozi wa Tanzania nchini Italia, Mheshimiwa James Msekela, pamoja na marafiki mbalimbali wa marehemu James A. Mbwana, walikusanyika kwenye misa takatifu ya kuuaga mwili wa  marehemu aliyefariki gafla jumatano tarehe 16 mei 2012 maeneo ya Termini mjini Roma akiwa njiani kuelekea Chuoni kama ilivyokuwa kawaida yake. 

Misa hii imefanyika katika parokia ya Mtakatifu Francisco jimboni Palestrina mjini Roma ambako marehemu alikuwa akitumikia na kuishi sambamba na kufuatilia masomo yake katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino kilichopo mjini Roma.  Misa iliongozwa na Mhasham Askofu Dominic, Askofu wa Jimbo la Palestrina.

Habari zaidi juu ya lini mwili wa marehemu utaondoka tutawapatieni kadri tutakapo zipata. Kwa niaba ya Jumuiya ya Watanzania Roma tunawapa pole sana ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mkubwa ambao unatukumbusha kuwa sisi binadamu hapa duniani ni wapita njia tu. Siku yoyote mwenyezi Mungu anaweza kutuchukua. Kwa hiyo hatuna budi kujiandaa kwa kusali na kutenda mema mbele ya mwenyezi Mungu.
 Bwana ametoa, bwana ametwaa jina lake liidimiwe milele amina! 
     Jeneza la Marehemu Fr. James Mbwana likiwa kanisani wakati wa misa.
   Kutoka Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mh. James Msekela pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Roma Mh. Leonce Uwandameno wakati wa ibada takatifu.
   Ibada ikiendelea. 
Kwa habari zaidi tafadhali tembeleeni

0 comments: