Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Thursday, August 31, 2017

TIMU YA JWTZ YAENDELEA KUNG'ARA KATIKA MICHEZO YA WAKUU WA MAJESHI WA AFRIKA MASHARIKI MJINI BUJUMBURA, BURUNDI


Timu ya Mpira wa kikapu  ya JWTZ  ikiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuwafunga mabingwa wa mwaka jana Ulinzi Kenya kwa vikapu 68-58 jana mjini Bujumbura, Burundi.
Kiongozi wa safara wa timu ya JWTZ ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMATA) Brigedia Jenerali Martin Amos Kemwaga akifurahia ushindi wa timu ya mpira wa kikapu jana mjini Bujumbura, Burundi.
Kiongozi wa safara wa timu ya JWTZ ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMATA) Brigedia Jenerali Martin Amos Kemwaga akihojiwa na mwandishi wa ITV wa Bujumbura Bw. Balen.

Timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) imeendelea kung’ara katika Mashindano ya muhula wa nne wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi wa nchi za Afrika Mashariki yanayofanyika mjini Bujumbura, Burundi. 
 Baada ya jana timu ya Mpira wa kikapu ya JWTZ kuwafunga mabingwa watetezi Ulinzi Kenya kwa vikapu 68-58, mori wa vijana wetu uliochagizwa na kauli mbiu ya HAPA KAZI TU, ulipanda tena leo katika mpira wa kikapu ambapo vijana hao hodari wa CDF Mabeyo wameibugiza Burundi kwa vikapu 94-18 bila huruma.  Na katika kabumbu pia JWTZ iliibuka kidedea kwa kuwapiga tena Warundi kwa mabao 2-1. 
“Tunashukuru Mungu kwa matokeo hayo yote”, mkuu wa msafara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMATA) Brigedia Jenerali Martin Amos Kemwaga, ameiambia Globu ya Jamii leo kwa njia ya mtandao. 
Brigedia Jenerali Kemwaga, ambaye yeye mwenyewe ni mchezaji nguli wa zamani wa mpira wa kikapu, ameeleza kufurahishwa na vijana wake ambao wamekuwa tishio katika michezo yote wanayoshiriki. 
Kaulimbiu ya Mashindano hayo ni “Shiriki michezo kama sehemu ya kazi, Kulinda Afya zetu na Kudumisha Mshikamano”, na yanahusisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na wenyeji Burundi. 
Timu ya JWTZ daima imekua ikifanya vizuri kwa kuchukua nafasi ya ya tatu kwa ujumla kati ya nchi zote zilizoshiriki katika mashindano yaliyofanyika hapo awali. Na safari hii timu hiyo kabambe imepania kunyakua nafasi ya kwanza kwani wao kila walipo ni HAPA KAZI TU.


0 comments: